Polisi wakagua nyumbani kwa Erick Kabendera, waondoka na hati yake ya kusafiria na nyingine za ndugu zake

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imefanya ukaguzi katika makazi ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera na kuchukua vitu mbalimbali ikiwamo paspoti saba za kusafiria.

Ukaguzi huo ulifanyika jana Jumatano Julai 31, 2019 nyumbani kwa Kabendera, Mbweni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na baada ya ukaguzi huo, mwandishi huyo alirudishwa ofisi za Uhamiaji, Kurasini.

Silinde Swedy ambaye ni wakili wa Kabendera akizungumza na Mwananchi jana Jumatano Julai 31, 2019 mara baada ya shughuli ya ukaguzi kumalizika alisema ukaguzi huo ulianza saa 9 alasiri na kumalizika saa 10 jioni.

Alisema katika ukaguzi huo, maofisa wa uhamiaji, “Walichukua paspoti saba za kusafiria.”

Mwananchi lilipotaka kujua hizo paspoti saba zote ni za Kabendera, wakili huyo alisema, “hapana, bali pasipoti moja ni ya kwake (Kabendera) na zingine ni za ndugu zake zilizokutwa kwake.”

Pia, Silinde alisema wamechukua vyeti mbalimbali vya Kabendera.

Awali jana asubuhi, Kamishna wa Uraia na Paspoti wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, Gerald Kihinga akizungumza na Mwananchi alisema wanaendelea na mahojiano na mwandishi huyo kuhusu uraia wake.

Kuhusu uraia wa ndugu zake, Kihinga alisema watakapomaliza naye mahojiano watakachobaini ndiyo kitakachowafanya kuanza uchunguzi kwa ndugu zake.

Julai 29, 2019, watu waliojitambulisha ni askari polisi waliokuwa wamevalia kiraia walimchukua kwa nguvu nyumbani Mbweni.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Lazaro Mambosasa alisema waliamua kwenda kumkamata mwandishi huyo baada ya kutumiwa wito wa kufika kuhojiwa lakini akakaidi.
 
Waramba viatu mna tabu sana,baada ya kubumburuka utekaji sasa mnajitahidi kupika kila uchafu!!

Uhamiaji wamecchukua passport yake moja na wakachukua na za ndugu zake passport 6 walizozikuta kwenye makazi yake vikiwemo na vyeti vyake vya shule,ila heading imeandikwa kuwasafisha watekaji na wauaji!!
 
Naona wamebuni mbuni mbuni mbinu. ... nitarudia sehem hiyo.....
This too shall pass!
 
Wewe mtoa uzi huu mbona umeutoa bila ya kuufanyia utafiti ili kujua Facts zake?hizo passport saba ni za kwake binafsi?za ndugu zake?je zote hizo zilikuwa valid?AND why systems ya uhamiaji ilishindwa to pick him kuwa tayari ana hati nyingine ya kusafiria?(au ndio matokeo ya kuishi in a pit hole country),je hizo passport zote ni za Tanzania au zipo za nchi nyingine?please next mtoa uzi jazia nyama zaidi kwenye mada yako.Mwananchi mie sio msomaji wao hasa baada ya kumtosa mwandishi wao Azory,angalia Television ya ALJEEZERA bado inawapigania waandishi wao wanaoshikiliwa pale Misri,habari za kupotea kwa Azory haziandikwi kabisa kwenye gazeti alilokuwa analifanyia kazi.woga umeliingia gazeti hili linalojiita ni huru!1
 
Waramba viatu mna tabu sana,baada ya kubumburuka utekaji sasa mnajitahidi kupika kila uchafu!!

Uhamiaji wamecchukua passport yake moja na wakachukua na za ndugu zake passport 6 walizozikuta kwenye makazi yake vikiwemo na vyeti vyake vya shule,ila heading imeandikwa kuwasafisha watekaji na wauaji!!
Na we mramba visigino umeandika kumsafisha nani? we ndo ulomkagua mbona wajifanya kujua zaidi ya wenye kazi zao!?
 
1564642063043.png
 
We ndo umeongea la maana
Waramba viatu mna tabu sana,baada ya kubumburuka utekaji sasa mnajitahidi kupika kila uchafu!!

Uhamiaji wamecchukua passport yake moja na wakachukua na za ndugu zake passport 6 walizozikuta kwenye makazi yake vikiwemo na vyeti vyake vya shule,ila heading imeandikwa kuwasafisha watekaji na wauaji!!
 
Waramba viatu mna tabu sana,baada ya kubumburuka utekaji sasa mnajitahidi kupika kila uchafu!!

Uhamiaji wamecchukua passport yake moja na wakachukua na za ndugu zake passport 6 walizozikuta kwenye makazi yake vikiwemo na vyeti vyake vya shule,ila heading imeandikwa kuwasafisha watekaji na wauaji!!
alizipata wapi?!
 
Nilitaka ku comment ila kichwa cha habari na maelezo tofauti kabisa, sasa passpoti saba za ndugu zake kwa nini wasikamate wenye hizo passport?
Nani alikwambia kua uhamiaji wana shida na ndugu zake? Tabgu juzi usiku familia ha Kabendera ilitahadharishwa kua jana watakuja kucanya upekuzi nyumbani kwa kabendera. Nadhani ndu walipuuzia.
 
hao ndugu nao very bogaz,ilitakiwa kila mtu awe keshachukua paspoti yake baada ya kujua tu kwamba eric yuko lokapu kwa ishu za uhamiaji
 
Back
Top Bottom