Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,119
- 1,570
Yer 42:10 SUV
[10] Ikiwa mtakaa bado katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang’oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.
Kuna wakati unatamani kuondoka eneo fulani ulipo, ila unasikia sauti ya ndani inakuonya, au inakusisitiza usiodoke hapo, au unasikia moyo wako mzito kufanya hayo maamuzi yako.
Wakati mwingine unaweza ukawa ni uzito wa ki-Mungu, na wakati mwingine unaweza ukawa ni uzito wa adui shetani kukuzuia usiende pale Mungu amekuandalia ufike.
Napenda leo tujifunze kupitia ujumbe huu, ninaamini utaondoka na maarifa ya kukusaidia, hasa kama upo njia panda kwa sasa, ama kama utakutana na utata kama huu siku za mbele.
Ujumbe huu wa Mungu ulikuja kupitia kinywa cha nabii Yeremia, uliwataka Waisraeli kutokimbilia Misri baada ya kuanguka kwa Yerusalemu.
Mungu aliwaagiza wakae kwenye nchi yao, hakuna kukimbilia sehemu nyingine, hakuwaagiza wakae tu, aliwapa ahadi ya kuwajenga na kuwapanda ikiwa watatii agizo hilo.
Baraka ya Waisraeli ya kujengwa na kupandwa ilitegemea kukaa kwao katika nchi yao, ambapo wakati huo ilionyesha haikaliki, walichotamani wao ni kuondoka na kwenda nchi nyingine.
Hii inaweza kutusaidia hata kiroho, wakati tunaona hatupati zile baraka alizotuahidia Mungu tukiwa ndani ya Kristo, ndio wakati ambao tunapaswa kukaa vizuri ndani ya Yesu.
Yn 15:4 SUV
[4] Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Hili linapaswa kukaa kwenye moyo wako na fahamu zako, baraka za Mungu zinapatikana ndani Kristo, hata kama kwa sasa unaona mambo hayaeleweki, endelea kutulia kwake, tii neno lake, ishi kutokana na neno lake.
Sasa tukirudi upande mwingine, unaweza kukutana na hali ya kutaka kukimbia nchi yako, au eneo lako la kazi, au makazi yako uliyozoea, au biashara unayofanya, au kozi uliyosomea. Lakini ndani yako unakosa amani juu ya uamuzi huo unaotaka kuufanya.
Kama Waisraeli walivyoonywa wasiondoke kwenye nchi yao, hata kwetu tunaweza kukutana na onyo hili, hupaswi kukimbia eneo lako, Mungu anajua kwanini amekuweka hapo au amekuacha uwe hapo, anajua utabarikiwa ukiwa hapo hapo.
Mazingira yanaweza kukuonyesha huwezi kufanikiwa ukiwa hapo au huwezi kufikia ndoto zako ukiwa eneo hilo, ila kwa Mungu inaweza ikawa inaonekana tofauti kabisa na unavyoona wewe.
Kabla ya kufanya maamuzi ya kuondoka eneo moja na kwenda lingine, hakikisha unapata kibali cha Mungu, akikuambia kaa hapo hapo tii usiondoke.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana