unazungumziaje mechi ya leo mkuu!unaonaje nusu fainali tutapita kweli?
game la Valencia na Basel linaendelea hapa
Na Basel washapunguzwa kwa red card
Doh!basi tena
Wanahitaji kujishika sana ili wafike kwenye matuta, maana kucheza mkiwa 9 wenzenu wameenea, lazima ulale na Aspirin
Mkuu kwa kweli nilikua naangalia highlights za Sevilla Vs Porto, kwa kweli wamenitisha kidogo kwa namna walivyokua wanashambulia kama mbwa mwitu toka dk ya 1
Kama tutakutana na Sevilla au Valencia/Basel (nadhani game bado inaendelea) nina uhakika wa kufika fainali,
Benfica ndio team ngumu sana, iko stable kwa muda mrefu, ina msimu mzuri domestically na wana uzoefu na kombe hili, halafu wanacheza mpira ambao huwa unatupa shida sana Juventus, wanajaa sana nyuma, ukuta mgumu, wanashambulia kwa kushtukiza na wana mawinga wanakimbia kama kicheche. Itabidi tuwe kwenye kiwango cha juu kuwafunga hawa.
Ndio maana naomba kukutana nao kwenye fainali, kwa sababu tutakua na extra motivation ya kushinda match
Haya wandewa, tumepewa Benfica FC na tunaanzia kwao, tukivuka hapa kombe letu
shifta juve2012 Ziroseventytwo pachanya
na kule nae Sevilla anaanzia kwao kisha anaenda Mestalla...ok hayatuhusu haya ni ya kwao.
Turudi kwetu.
Sie tunaanzia kwa yule ndege anaezunguka uwanjani...dah pale sasa ndo pa kwenda piga mipango maridhawa na kupata ya ugenini kisha shughuli twaja imaliza Juventus Stadium...
Naam,scudetto ileeee!Tupo wanabianconeri kama kawa kama dawa tunaendelea kutoa dozi
Mpaka sasa Udinese washachutama mara mbili
Naam,scudetto ileeee!
Umemuona yule "panya" wako anavyokatiza chini ya makwapa ya mabeki?
Hapana mkuu.sijatazama Leo