Jumuiya ya Afrika mashariki imeonyesha udhaifu mkubwa kwenye suala la EPA,,

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
siku za hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kati ya nchi zinazounda Afrika mashariki kuhusu kutia sahihi mkataba wa EPA au kutoweka sahihi mpaka baadhi ya vipengele ziwekwe sawa.Nchi ambazo bado hazijaweka sahihi ni Tanzania&Uganda lakini Uganda anaonyesha wazi anakubaliana na mkataba huo na serikali ya Museveni inaishawishi uongozi wa Magufuli utie sahihi mkataba huo,Tanzania bado hawaikubali EPA na saizi kumekuwa na tension kubwa kuhusiana na ushirikiano na umoja wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,kama hakuna kauli moja,ushirikiano katika suala sensitive kama hili basi ni dhahir shahir muunganiko huu hauna maana na tija ni kama vile povu kwenye bahari.

kwanini nchi za Afrika mashariki hazina kauli moja,umoja&ushirikiano.Moja ya sababu ya umoja wa Afrika mashariki kuundwa ni kudumisha umoja&ushikamano na kuwa na kauli moja lakini hali imekuwa tofauti,kwenye maamuzi ya pamoja kila mtu anakuwa na kauli yake

Nimekumbuka ushirikiano&umoja waliokuwa nao viongozi wa Latin Amerika ,walikuwa na kauli moja na ushirikiano wa karibu na walikuwa hawana ubinafsi.Rais Evo Morales,Hugo Chavez,Lura Da Silva,Nestor Kirchner

Mwaka 2005 wakati G.Bush alienda bueno aires kukutana na viongozi hawa ili wasaini mkataba wa FTAA kati ya nchi hizi na USA kuruhusu ''free trade'' ,viongozi hawa walisimama kidete kupinga&kukataa mkataba huo uliojaa ukandamizaji na kuwatajirisha USA na walimuambia Bush aondoke

viongozi wa Afrika mashariki wakutane na wafanye mkutano wa pamoja na kuamua moja na siyo kila nchi ijiamulie tu na kulazimishana kutia sahihi bila ya kupitia mkataba na kuangalia interests za EAC,kama kwenye suala kama hili kumekuwa na sintofahamu basi pasi na shaka naamini umoja huu na mikutano inayofanya Arusha ni hewa na hayana umuhimu wowote ule.










 
Back
Top Bottom