Jumanne ni siku ya ajabu kibiashara

Jumanne ni siku ya ajabu kibiashara

Papi Chulo

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
6,260
Reaction score
7,397
Wadau nina miaka 9 kwenye vi-biashara vyangu vya hapa na pale, lakini tangu zamani huwa naishangaa sana hii siku ya Jumanne, biashara inaweza kuwa mbaya na kusuasua siku zote, lakini ikifika tu Jumanne kudadeki yaani napiga biashara hadi najiuliza hivi MUNGU ameweka kitu gani katika hii siku

Jamani kuna siri gani katika siku hii ya Jumanne, yaani haijawahi niangusha toka kitambo hicho cha umachinga hadi leo hii...
 
Nadhani kwajinsi siku za juma zilivyo jipanga, hicho ndicho chanzo likubwa kwa siku ya juma nne biashara kutoka kwa wingi kuliko siko zingine....
Kwamfano:-

Mwisho wa juma hapa Tz ni ijumaa, na ijumaa watu wengi wanapo toka kwenye mihangaiko, pamoja na kuswali... wengi hukua wachovu na wengine huwai nuumbani kwa familia na wengine hukimbilia sehemu na maeneo mengi tofauti kwaajili ya kujipumzisha ama kupata starehe kidogo, na hapo ndipo unakuwa mwisho wa siku ya ijumaa.

Juma mosi ni siku ambayo watu wengi hukuwepo tu nyumbani na familia, ama hufanya usafi wa nyumbani na nguo. Na siku hii wengi hukaa nyumbani kupika&kula pamoja na fimilia na siku hii kuisha namna hiyo.

Juma pili watu wengi huifanya ya kuwenda kwenye ibada, na kutembelea ndugu jamaa na marafiki, pia siku hii wapenzi wengi huitumia kitembeleana na hata familia nyingi hutoka pamoja na watoto ku hang around.

Juma tatu ni siku ngumu sana kwa watu wengi kwasababu wengi huwa bado na uchovu/mning'inio wa jana yake, na watu wengi huwa na kazi nyingi kwasababu ya long weekend pamoja na viporo vya kazi zilizo salia wiki jana. Siku hii huwa imekaa kimikakati zaidi sabaabu ya gape ambalo linakuwa limejitokeza nyuma yake.

Juma tatu ni siku ngumu kwasababu ya pressure ya kutaka kufikia malengo ya wiki nzima ilio anza siku hiyo, na hivyo watu wengi huwa busy sana.

Kwa maelezo hayo mkuu bilashaka unaweza ukaelewa kwamba kwanini siku wa jumanne ndipo biashara yako hutoka zaidi kuliko siku zingine zote, na sababu kubwa ni kwamba juma nne ndipo watu wengi hupata nafasi ya kufanya manunuzi na kupata mahitaji kwaajili ya wiki nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom