Jumamosi ya usafi imekuwa siku ya wafanyabiashara kupumzika

kintu

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
540
133
Kama ilivyo kawaida jumamosi ya mwisho wa mwezi imekuwa ni siku ya usafi na wafanya bihashara wamekuwa wakifunga bihashara zao kwa ajili ya kushiriki usafi na kufungua kuanzia saa 3.

Lakini ukipita maeneo mengi utaona maduka yamefungwa na hakuna watu wanaofanya usafi katika maeneo yao. Leo nimepita mwenge na kuona maduka yamefungwa na maeneo ya nje yakiwa machafu na hakuna watu wakiendelea zoezi la usafi. Hii ina maana wafanyabiashara wanakaa nyumbani kusubiri saa 3 wafungue.

Nashauri watendaji wa serikali waendelee na moto waliokuwa nao mwanzani ikiwa na kutoa faini kwa wale wasioshiriki zoezi la usafi katika maeneo ya bihashara zao.
 
Huyu nae vipi kavurugwa nn nahisi atakuwa hajapata mshahara baba mkumbushe tajiri wako Leo mwanzo wa mwezi
 
Yap ni kweli hili zoezi limekosa maana halisi ila wanachonikera ni kutaka hata yale maduka ya mitaani yafungwe wakati wenye nyumba hufanya usafi kila cku hii iwe kwenye maeneo ya maduka mengi
 
Back
Top Bottom