Juma ubao, toma toma, matimila.

Juma ubao, toma toma, matimila.

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
1,241
Reaction score
253
Wadau wa muziki wa wa dansi. Kuna nyimbo nimezikumbuka za siku nyingi kama kuna anayeweza kuweka hapa jamvini itakuwa faraja iliyoje kwangu, maana sijui jinsi ya kuzipata ukizingatia siku hizi bongo fleva imetawala.

1. Mwanaidi:uliimbwa na bendi ya toma toma.
2. Alimasi: Uliimbwa na bendi ya super matimila.
3. Mshenga: Uliimbwa na juma ubao-kwenye wimbo huu juma ubao aliimba, kapiga kinanda, solo gitaa,sax
 
Nimetokea kumpenda binti mwanaidi.......Hizo nyimbo tamu sana kamanda, sijaona tena
 
Mkuu huo wimbo na.3 juma ubao nilimsikia akihojiwa akisema kipindi hicho redio ya kurekodi nyimbo ilikuwa moja tu rtd. Wakashangaa mbona hukuja na wapigaji wa kutosha? Kawaambia anao uwezo wa kupiga chombo zaidi ya kimoja kwenye wimbo mmoja, kipindi hicho teknolojia ikiwa bado. Kweli juma ubao namkubali, hivi yuko wapi?
Nakumbuka baadhi ya maneno ya wimbo...mshenga wako kakamatwa ashitakiwe kama mwizi....waliuliza ushahidi uko wapi...makusa...
 
Nimetokea kumpenda binti mwanaidi.......Hizo nyimbo tamu sana kamanda, sijaona tena

KWELI HUO WIMBO MTAMU, NILIUSIKIA JANA KWENYE DALA DALA. "MIMI NAJUTA EEE! NAJUTA MAAMA, GHARAMA NILIZOMGHARAMIA AMEONA BUURE! SHAMBA SINA MIFUGO SINA, SIJUI LA KUFANYA MWANAIDi!"
 
Wadau wa muziki wa wa dansi. Kuna nyimbo nimezikumbuka za siku nyingi kama kuna anayeweza kuweka hapa jamvini itakuwa faraja iliyoje kwangu, maana sijui jinsi ya kuzipata ukizingatia siku hizi bongo fleva imetawala.

1. Mwanaidi:uliimbwa na bendi ya toma toma.
2. Alimasi: Uliimbwa na bendi ya super matimila.
3. Mshenga: Uliimbwa na juma ubao-kwenye wimbo huu juma ubao aliimba, kapiga kinanda, solo gitaa,sax

Wasiliana na Waandaaji wa vipindi wa Muziki wa Zamani katika Radio zetu zote za FM...Wana collection kali hadi utashangaa
 
Kushoto ni Kawele Mutimuana aliyepiga solo katika kibao Mwanaidi kilichorekodiwa RTD mwaka 1982. Hapa anatoa somo la upigaji solo. Hii ni mwaka 2011 nchini Uingereza, ambako ndiko anakoishi kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:

kushoto ni kawele mutimuana aliyepiga solo katika kibao mwanaidi kilichorekodiwa rtd mwaka 1982. Hapa anatoa somo la upigaji solo. Hii ni mwaka 2011 nchini uingereza, ambako ndiko anakoishi kwa sasa.

so nice
 
Last edited by a moderator:

Wimbo: Mwanaidi
Bendi: Orchestra Toma Toma
Mwaka: 1982
Waimbaji: Kasaloo Kyanga, Skassy Kasambula, Banza Tax
Solo: Kawele Mutimuana
Drums: Abuu Semhando "Lokassa"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom