Juma Nkamia: Mnataka muonekane kwenye TV watu wazima kwani mnatafuta wachumba?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,798
Kupitia kipindi cha usiku cha bunge TBC tumekusikia Juma Nkamia ukichangia hotuba ya Waziri mkuu.

Ukweli huna lolote la maana kwa manufaa ya jimbo lako moja ya majimbo masikini sana ulilochangia zaidi ya kujikomba pangine ukidhani utapewa tena unaibu waziri ufukie mashimo baada ya kuwa failure ulipoupewa.

Kubwa zaidi ambalo ndio msingi wa mada hii na linalodhihirisha yale maneno aliyowahi kusema Tido Mhando kuashiria kuwa hukuwa mwandishi BBC bali kanjanja presenter ni pale ulipokuwa unawakejeli wabunge tuliowatuma kuwa tunataka kuona nini kinaendelea Bungeni bila kuchujwa.

Kwa kauli yako ulisema "Mnataka muonekane kwenye TV watu wazima kwani mnatafuta wachumba?"

Hapo ndio nilipoamini kuwa pamoja na kupelekwa BBC ukasome habari umeshindwa kujifunza kwa vile kweli ni Kanjanja.

Nadhani hata wabunge wenzako wa CCM wanaojielewa wamekushangaa na ndio maana walikuwa wanakutolea macho tuu.

Unashindwaje kujua mahitaji ya RAIA kujua nini kinaendelea ndani ya bunge lao? Au hutaki watu waone pumba unazochangia kama za Leo?

Kwa style yako hiyo jimbo LA Nchemba kupata maendeleo ni ndoto
 
maeneo ya kondoa na dodoma ni shamba la bibi , hivi mnaacha watu makini mnachagua mtu muongo kama nkamia ! huyu alipewa deiwaka BBC kwa sababu ya kujua kiswahili ili asome taarifa ya habari kwa dk 10 tu kisha aondoke lakini akadanganya eti kaajiliwa , mtakula magunzi na viwavi hadi mkome .
 
Mahitaji ya raia ni kupata huduma safi za kijamii n.k na sio kuonesha wabunge wakiongea live...

Bilioni 4 zipelekewe vijana wajiajiri...
Labda RAIA viazi, lakini wale making wanataka kujua kila kitu nao waelewe nini kinaendelea katika maeneo yao. Ona Leo waneshindwa hata kupata kwa uhakika PM wao kasema nini kama dira yake.
 
maeneo ya kondoa na dodoma ni shamba la bibi , hivi mnaacha watu makini mnachagua mtu muongo kama nkamia ! huyu alipewa deiwaka BBC kwa sababu ya kujua kiswahili ili asome taarifa ya habari kwa dk 10 tu kisha aondoke lakini akadanganya eti kaajiliwa , mtakula magunzi na viwavi hadi mkome .
Hahahahaha
 
Kumbe na wewe unaangalia Bunge usiku? Makubwa.
Nitapataje moral authority ya kusema kinachofanywa na TBC ni usanii kama sijaangalia?
Sasa ndio nimeona jinsi mambo yaliyofanyika kuanzia saa 4 hadi saa 7 na saa11 jioni hadi saa 2 usiku jumla masaa 6 na kuwa complied to one hour.
Hiyo ni ratio ya kila zile dakika 10 zinaweza kugeuzwa kuwa dakika 1 sekunde 40
 
Yaani unapoteza lisaa lizima hivi hivi?
 
Back
Top Bottom