kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,098
Nakumbuka mwaka 2001 kwenye chati ya nyimbo kumi za Bongo Fleva kwenye kituo cha Radio One Stereo, pale mtangazaji wa kipindi hicho alipoitangaza ngoma iliyoshika nafasi yakwanza.Mtangazaji, Godwin Gondwe aka Double D aliutambulisha kwa umaridadi mkubwa wimbo wa Mike Tee aliomshirikisha Juma Nature,Nampenda. Hadi leo naikumbuka siku hiyo.
Naipata picha ya jinsi nilivyokuwa pembeni ya redio yangu nikiusikia wimbo huo. Nakumbuka hisia nilizopata za kusikia wimbo huo mtamu wa Bongo Flava.Nature alikuwa muuaji wa chorus enzi hizo na kwakweli ulikuwa ukimshirikisha Nature kwenye ngoma yako, uhakika wa kutengeneza hits ulikuwa ni asilimia 100.
Sikiliza kwenye Zali la Mentali alichokifanya kwa kumpa Profesa Jay miongoni mwa chorus kali kuwahi kuimbwa kwenye muziki wa Bongo Flava. Sikiliza Gado ya Zay B, Hatuna Fedhaya Richie One, Nenda ya Chege, Msela ya marehemu Ngwair, Ndio Mzee ya Profesa Jay na zingine kibao. Nature alikuwa mnyama wa viitikio.
Nature alikuja na mtindo wa uandishi wa Kiswazi, rap katuni na uwezo mkubwa wakutengeneza melody. Uwezo wake wa vitu hivyo vitatu na zaidi unadhihirika kwenye nyimbo kama Jinsi Kijana katika mdundo wenye hisiakali. Ama sikiliza kile alichokifanya kwenye Sitaki Demu. Nature alikuwa hahitaji mtu wa kumfanyia chorus, alikuwa jeshi la mtu mmoja.Mpe beat kali mengine mwachie mwenyewe.
2002 kama sikosei, Nature alifanya vizuri nawimbo ‘Inaniuma Sana’ alioimba kwa hisia nakudaiwa kuwa ni wimbo aliomtungia ex wake,Sintah japo mashairi aliyoimba yalikuwa yakisanii zaidi. Ni wimbo wa utani lakini unaovutia masikioni na wenye ujumbe mzito. Na hakuna anayeweza kuisahau chemistry yake na P-Funk Majani.Kighetogheto ni wimbo mwingine uliozitesa spikaza redio enzi hizo. Ikiwa na beat kali ya mdachi na chorus yake ikiwa na sauti za chini za Mr Paul, ngoma hii ilikuwa ya kukufanya usimame iishe kwanza pale ulipoisikia ikichezwa sehemu.Vipi Hili Game? Ni wimbo wa kusababisha uchiz ikila unapousikia – lazima uinuke, ucheze. Ni wimbo wa kufungia show na kuwatoa jasho mashabiki pale anapokuwa akiutumbuiza.
Kipindi Nature yupo kwenye chati, mpinzani wake mkubwa alikuwa Inspekta Haroun. Tension yao ilitokana na mitindo yao ya rap katuni, rap yenye melody, matumizi ya maneno ya uswahili na wote kutokea Temeke. Lakini tofauti zao ziliisha baada ya kufanya pamoja wimbo remix ya Mzee wa Busara. Nadiriki kusema hii ni miongoni mwa collabo kali za Bongo Flava na Majani alithibitisha ujiniazi wake kwenye midundo.
Nature ni miongoni mwa rappers wenye hits nyingi kuwahi kutokea na mchango wake kwenye muziki wa Bongo Flava haupwaswi kusahaulika.Mafanikio yake hayakuishia Tanzania tu bali aliwahi kushinda tuzo za kimataifa ikiwemo Channel O Music Video Awards – Best African East mwaka 2007.Mwaka huo, alitajwa pia kwenye MTV Europe Music Awards – Best African Act. Hadi sasa ana album tano, zikiwemo Nini Chanzo (2001),Ugali(2003), Ubinadamu-Kazi (2005) Zote History(2006), Tugawane Umaskini (2009).Sir Nature ni madini kwenye Bongo Flava.