rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,359
- 22,516
Juma Abdul aonyesha umbo lake dogo halimzuii kutembeza ubabe, apambana na Banda wa Simba..
Beki Juma Abdul wa Yanga ndiye amekuwa gumzo zaidi mitandaoni kutokana na kuonyesha ubabe wake.
Abdul anaonekana kwenye picha akijaribu kumkaba beki wa Simba, Abdi Banda licha ya kwamba ana umbo kubwa kuliko yeye.
Beki huyo wa Yanga, alivaana na Banda wakati wa mechi hiyo ya watani hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana.
Vurugu lilianza baada ya Banda kumuangusha Kaseke ambaye alionekana kuumizwa kutokana na hali hiyo, Abdul akamvaa Banda na kuanza kumvinya usoni.
Hata hivyo, baadaye mwamuzi wa mchezo huo aliwaramba kadi za njano wote wawili kwa hatua hiyo.
Ukiangalia inaonekana Abdul ana umbo sana ukimlinganisha na Banda. Lakini inaonekana hakujali na alitaka kuonyesha yeye ni ‘msela’ wa Tandale na hataki mchezo hata kidogo.
Mechi hiyo iliisha kwa suluhu ndani ya dakika 90. Mwisho Simba ikashinda kwa mikwaju 4-2 ya penalti na kusonga fainali.
My Take:
Ukiisoma hii habari ndio unajua upeo wa waandishi wetu ukoje. Badala ya kuonya tabia mbovu za wachezaji hapa wanamsifia Juma Abdul akisoma hii habari ataona kama kafanya kitu cha maana atarudia tena akipigwa red card ataona kaonewa wakati Abdul Banda akisoma hii habari atakuwa anapanga kulipiza kisasi.
Waandishi wetu wanapaswa kuwa makini na kile wanachoandika.