Julius Malema, Nyota inayong'aa kuliangaza bara la Afrika

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Huyu ni kijana ambaye ambaye kwa kweli maisha yake ya siasa yanapitia katika mitihani migumu sana kumfananisha na Rais wa kwanza wa tsifa lake hayati Mzee Madiba na hayati Patrice Lumumba wa DRC.Katika pitia pitia zangu za watu maarufu waliowahi kuonesha misimamo thabiti na kupitia katika hali ngumu ya maisha yao ya siasa wakiwa wangali vijana wabichi kabisa ni Madiba na Lumumba.

Julius Malema alikua kiongozi mkuu wa jumuiya ya vijana wa chama tawala ANC ya S.Africa, alionesha misimamo kwa aliyoyaamini yeye has a kupinga Ufisadi! Sio mtu wa kijipendekeza wala kujikosha kwa watawala,anajiamini na alipingana wazi wazi wazi na Mkuu wa nchi yake hali iliyomfanya kufukuzwa ndani na kuandamwa na na serikali ikiwa ni pamoja nakumshtaki kwa kashfa mbalimbali ambazo mpaka Leo yeye anadai zilikua za kutengenezwa.

Ilifikia mahali Julius Mapema, alinyanga'anywa hadi samani zake zote za ndani ya chumba alichokua akiishi na kuachiwa nguo za kuvaa tu! Aliishi katika maisha magumu sana ya kuomba omba hata pesa ya kula baadae ya kufukuzwa ANC.Pamoja kuandamwa na vyombo vya dola vya nchi hiyo lakini Malema aliendelea kusimamia anachokiamini na kuanzisha chama chake cha siasa kijulikanacho kama Economic and Freedom Fighters(EFF) ambacho kwa sasa ni chama cha siasa kinachokua kwa kasi S.Africa na kuonekana kua tishio kwa serikali ya ANC.

Julius Malema na chama chake kichanga sasa kina wabunge zaidi ya 20 ndani ya bunge la nchi hiyo, ni wabunge ambao pamoja na uchache wao wanaonekana ni tishio kwa serikali ta ANC,Imefikia mpaka kuitishia srikali kwa kuiambia kua kama raia wataendelea kuuawa na vyombo vya dola basi nao watashika bunduki kukabiliana na hali hiyo.

Kwa sasa Malema na Chama chake wamefunguliwa mashtaka na serikali ya nchi hiyo baada ya ANC kuiomba serikali kumchukulia hatua yeye chama chake kwa matamshi hayo ambayo wamedai ni hatari kwa usalama wa taifa.

Julius ni aina ya mwanasiasa kijana ambaye hajawahi kurudi nyuma kwa misimamo yake, anaendelea kupata uungwaji mkono na makundi mkubwa hasa vijana nchini kwake.Huyu ni kijana mfano wa kuigwa na vijana wanasiasa Afrika, ni kijana ambaye kama Mungu atamlinda baade anaweza kulitetea bara hili ambalo umoja wake umekua ni bubu kwa masuala mengi kwa jamii za kiafrika.
 
Sio tu mwanasiasa kijana Bali pia ana Elimu ndogo Na hakuwa Na akili sana darasani!ila Kwasasa Ni moto wa kuotea Mbali Kwa serikali ya ANC
 
Sio tu mwanasiasa kijana Bali pia ana Elimu ndogo Na hakuwa Na akili sana darasani!ila Kwasasa Ni moto wa kuotea Mbali Kwa serikali ya ANC
Mara nyingi amekua skimshtum Rais Jackob kwa kumita Zuma fisadi, Juzi Mahakama ikamuadabisha Zuma lakini influence ilitoka kwa Malema. Je,hapa Tz nani anadiriki kumsema Rais?
 
Mara nyingi amekua skimshtum Rais Jackob kwa kumita Zuma fisadi, Juzi Mahakama ikamuadabisha Zuma lakini influence ilitoka kwa Malema. Je,hapa Tz nani anadiriki kumsema Rais?

wanasiasa vijana wa kitanzania pamoja na watanzania kiujumla tuko kama shockup. wanasiasa ndiyo kabisaa wako kwa ajili ya maslahi yao
 
Mara nyingi amekua skimshtum Rais Jackob kwa kumita Zuma fisadi, Juzi Mahakama ikamuadabisha Zuma lakini influence ilitoka kwa Malema. Je,hapa Tz nani anadiriki kumsema Rais?

Hapa bongo wananchi hatutakiwi kujua chochote kile kibaya kinacho husu serikikali ndio maana Saa hivi hata bunge hatutakiwi kuangalia live
 
Ungeweka chanzo cha habari yako.

Malema hajawahi kuwa ombaomba na haitakaa itokee.

Yaani uwe rais wa ANCYL kwa miaka minne halafu uwe unaishi sijui kwenye chumba!!,hata Patrobas Katambi wa BAVICHA hawezi.

Kumbuka Malema a.k.a Juju alikuwa swahiba mkubwa WA Zuma na ndicho kipindi alichokitumia kuchuma.

Kwa sasa 2016 anakadiriwa kuwa na net worth ya $.2million pamoja na kwamba anazongwa na government.

Hebu niambie kazipata wapi kama 2012 alikuwa omba omba?
 
Tusibili wanaojua zaidi kuhusu malema watujuze kwa kina zaidi. Hata ivo nashukuru kwa mlivotufahamisha haya machache.
 
Jamaa Ni mpambanaji....! Wanabadiliko wetu hapa wanashindwa hata kusimamia halimashauri walizonazo mpaka wanapiga hati chafu.....!
 
Ungeweka chanzo cha habari yako.

Malema hajawahi kuwa ombaomba na haitakaa itokee.

Yaani uwe rais wa ANCYL kwa miaka minne halafu uwe unaishi sijui kwenye chumba!!,hata Patrobas Katambi wa BAVICHA hawezi.

Kumbuka Malema a.k.a Juju alikuwa swahiba mkubwa WA Zuma na ndicho kipindi alichokitumia kuchuma.

Kwa sasa 2016 anakadiriwa kuwa na net worth ya $.2million pamoja na kwamba anazongwa na government.

Hebu niambie kazipata wapi kama 2012 alikuwa omba omba?
Usiwe mvivu wa kufikiri wewe! Kua mtundu wa kufuatilia mambo, Malema aliwahi kunyang'anywa hadi TV na kitanda chake kwa madai kua alikua na mkopo hakulipa. Lakini zote zilikua ni njama za chama chake.
 
Back
Top Bottom