Julius Malema, angekuwa ni Mbunge katika Bunge letu sidhani kama angevumilia

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,323
152,127
Kwa yaliyotokea mpaka sasa,huyu angekuwa ni Mbunge katika Bunge letu bila shaka saa hizi angekuwa ameshatangaza rasimi msimamo wake wa ku-table motion ya kumvua mtu fulani madaraka yake.

Wenzetu hawa huangalia zaidi kutimiza wajibu wao bila kujali kuwa kuna watakaomkwamisha au kumzongazonga.

Huku kwetu hili ni jambo la ajabu kabisa na watu wanakuona kama mhaini!

Kinachonisikitisha na kunishangaza ni kuona wapinzani wetu wanakuwa wema na wavumilivu bila kujali wanayotendewa kiasi kwamba hawataki kumia rungu lao ku-hit back.
 
Kuna uongozi wa kimaslahi na uongozi wa kinadharia. Wetu wako kimaslahi zaidi
 
Tuna wabunge mahiri zaidi ya Malema bungeni, tatizo ni ubabe wa kuwanyamazisha tu, tumeshuhudia hata wakizimiwa vipaza sauti pale wanapojaribu kusema kweli na kukosoa uozo, tatizo ni mfumo unaotumika kuendesha bunge.
 
Hivi kwanini wakati wa kuomba kura wanakuwa wazuri kweli ILA wakikalia kiti mambo yanaanza kwa kuweka sheria kandamizi kama vile uhuru wa kutoa maoni unafungwa, uhuru wa vyombo vya habari nao umefungwa, sheria ya dhana potofu ya 'uchochezi' ili kuufunga umma midomo wafanye wayatakayo!
 
Kwa yaliyotokea mpaka sasa,huyu angekuwa ni Mbunge katika Bunge letu bila shaka saa hizi angekuwa ameshatangaza rasimi msimamo wake wa ku-table motion ya kumvua mtu fulani madaraka yake.

Wenzetu hawa huangalia zaidi kutimiza wajibu wao bila kujali kuwa kuna watakaomkwamisha au kumzongazonga.

Huku kwetu hili ni jambo la ajabu kabisa na watu wanakuona kama mhaini!

Kinachonisikitisha na kunishangaza ni kuona wapinzani wetu wanakuwa wema na wavumilivu bila kujali wanayotendewa kiasi kwamba hawataki kumia rungu lao ku-hit back.
Nakubaliana na wewe ktk misimamo ya Malema lakini hata angekuwa Tz asingefanikiwa kwasababu hizi nchi mbili mifumo ya uongozi iko tofauti na hata Katiba zake zinautofuti mkubwa sana.

Hata sisi tunaweza kupitia Bunge kuweka mezani hoja ya kutakuwa na Imani na Rais kama kanuni za kudumu za Bunge zinavyoainisha.

Issue ni Imani ya wanaotakiwa kulitekeleza hilo hawataweza kutokana na mifumo yetu ya ndani ya uongozi.

Hii ni nchi ambayo sivyo unavyoijua kwa nje.

Magufuli piga kazi heshima umeanza kurudi mtaani na salami tumeanza kupata sasa.
 
Back
Top Bottom