Julai 23 (J23): Kura za maruhani hazizuiliki,ujumbe utatumwa tu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,137
17,908
Hata kama chama kitajichora kama kilicho imara na pamoja,kura za maruhani hazitaepukika wala kuzuilika Dodoma. Makada wamejipanga kutuma ujumbe. Ujumbe wa kutokukubaliana na kukabidhi badala ya kuchagua Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.

Makada wanajipanga kutuma ujumbe wa kura za maruhani. CCM ina bahati moja. Hapa Dodoma, kura zitapigwa na wanaCCM,kuhesabiwa na matokeo kutangazwa nao wenyewe. Hata kura zisipotosha,zitatosha. Lakini,ujumbe utakuwa umeshatumwa kwa wakuu.

Karibuni Dodoma makada tutume ujumbe chamani mwetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
huku kwetu chadema cheo cha mwenyekiti hakiguswi, hakiruhusiwi kujadiliwa kabisa!!
Nkuruzinza wa Chadema alishanyofoa kipengele cha ukomo wa Madaraka na kina Kitila na Zitto walipojaribu kusema wakafukuzwa.
Atakabidhi madaraka kwa Mkwewe mtarajiwa (Mkaza Mwanae) 2030 kama yeye alivyokabidhiwa kwa Mkwewe Edwin Mtei.
 
Kura zitapigwa. Ni maigizo ya kawaida hapa Tanzania

Mzee Tupatupa
Mbowe hajawahi kugombea Uenyekiti wa Chadema na mtu yoyote. Ni mwendo wa yeye kutangaza uchukuaji wa form na yeye ndio ataongoza kamati kuu ya kuteua jina la mgombea na Kamati ya Wazee ikikutana Mwenyekiti ni Mkwewe. Lakin bado jina la Chama lina neno "Demokrasia" Bakita watusaidie kama ni halali kutumia hilo jina.
 
Mbowe hajawahi kugombea Uenyekiti wa Chadema na mtu yoyote. Ni mwendo wa yeye kutangaza uchukuaji wa form na yeye ndio ataongoza kamati kuu ya kuteua jina la mgombea na Kamati ya Wazee ikikutana Mwenyekiti ni Mkwewe. Lakin bado jina la Chama lina neno "Demokrasia".
CCM je?

Mzee Tupatupa
 
CCM je?

Mzee Tupatupa
John Magale Shibuda alishajitokeza kumkabili Dr.Jk kwny uchaguzi wa 2012 lakin kwa hekima zake akaona ajitoe atoe fursa kwa Jabali la Demokrasia na Uvumilivu wa kisiasa Afrika Mashariki na Kati Dr.Jakaya aendelee na harakati zake za kukomaza Demokrasia Tanzania.
 
Mbowe si aligombea kabisa na Mbaruku wa Tabora? Waonekana wewe ni mwanaCCM kiushabiki tu. Hujui lolote.Tangu kuanzishwa kwake,Uenyekiti wa CCM haukuwahi kugombewa

Mzee Tupatupa
 
John Magale Shibuda alishajitokeza kumkabili Dr.Jk kwny uchaguzi wa 2012 lakin kwa hekima zake akaona ajitoe atoe fursa kwa Jabali la Demokrasia na Uvumilivu wa kisiasa Afrika Mashariki na Kati Dr.Jakaya aendelee na harakati zake za kukomaza Demokrasia Tanzania.
Sasa hapo jibu ni lipi? Aligombea au hakugombea?
Maana hata zitto aliwahi kuchukua fomu lakini akaamua kumpisha Mbowe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom