Jukwaa la wakulima, wafugaji Kiteto laanzishwa

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Baada ya msuguano wa muda mrefu wa wakulima na wafugaji wilayani Kiteto Mkoani Manyara, kugombea ardhi kwaajili ya shughuli za kilimo wameamua kuanzisha jukwaa la wakulima na wafugaji.

Jukwaa hili litatumika kama chombo kitakachopunguza migogoro hiyo kwa kutumia uzoefu wa majukwaa mengine hapa nchini na ambayo yalifanikiwa.

Wajumbe wa jukwaa hilo ni wadau wanaotumia ardhi, kama vile wakulima, wafugaji, viongozi wa Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo.

Kikao cha jukwaa la wadau wa masuala ya ardhi kimeandaliwa na shirika la KINNAPA kwa kushirikiana na Jumuiko la maliasili Tanzania chini ya ufadhili wa Care Intenational wamekuja na mtazamo kupunguza migogoro ya ardhi Kiteto kwa kuwatumia wakulima na wafugaji wenyewe.

Baada ya wananchi kwa muda mrefu kudhani migogoro ya ardhi Kiteto itaondolewa na viongozi wa ngazi za juu, baada ya kutafakari wameina kuwa migogoro hiyo itaondolewa na pande hizo zinazohasimiana.

Wakishauri njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo baadhi ya washiriki, akiwepo Lembulug Koyando wa shirika la NAADUTARO Kiteto pamoja na wadau wa majukwaa mengine toka Iringa walipendekeza ili kuwe na fanikio washirikishwe wadau wote kuunda jukwaa hilo kama njia bora ya kujenga mahusiano na utatuzi wa migogoro hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda wakati wajumbe hao wakiendelea kujitafakari na kuongezwa kwenye jukwaa hilo huku Abrahamu Akilimali wa shirika la KINNAPA akiteuliwa kuwa mratibu.

Akizungumzia migogoro ya ardhi, Patrick Kimaro (Sabasiata) mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaya alisema, mbali na migogoro ya ardhi, haki kwa watoto wa jamii za wakulima na wafugaji kusoma zimeendelea kukiukwa.

"Kutwa mkulima yupo shambani mtoto anasoma saa ngapi! mfugaji anataka mtoto akachunge atasoma saa ngapi lazima haya yote yatazamwe" alisema Sabasita.

Imeelezwa kuwa jukwaa hilo ndicho chombo cha wadau wa ardhi kuzungumzia masuala yanayohusu ardhi likilengwa kuwa mwarubaini wa migogoro hiyo.

IMG-20191112-WA0026.jpeg
 
Back
Top Bottom