..Nadhani inawezekana hawakutumwa; isipokuwa wakati wa kutoa tamko lenyewe si muafaka! Wakati Jukwaa la Wahariri wanatoa tamko lenye hoja ya kuonyesha kwamba nchi ina rasilimali chache kulikuwa na haja ya kuangalia mambo haya:
- Kwa nini baadhi wa watumishi wa umma wanalipwa posho nono na kubwa kuliko kada nyingine?
- Kwa nini madaktari wagome ilhali wanalipwa vema na posho zao ni kubwa kuliko kada nyingine?
- Wabunge sawa; madaktari hapana na walimu pia hapana!
Kuna kila sababu ya kuangalia ukomo wa matumizi ya rasilimali kwa kuangalia uwiano wa mgao wake kwa kada zote zinazohitaji malipo ya halali na yanayokidhi mahitaji yao kiuchumi, kijamii na kisiasa! Tuangalie rasilimali kwa mtazamo wa mgawanyo wa uhuru, haki na usawa. Isiwezekane kwa kada moja kupewa nafasi ya kutumia zaidi ilhali kada nyingine wakiambia wajifunge mkanda (mkwiji) kukubali maumivu ya maisha.