sweetdada
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 518
- 170
Habari wadau.
Huu ni kama muendelezo wa hadithi ya maisha yangu ya kimahusiano ambayo nimewahi kuleta hapa MMU miaka kadhaa iliyopita. Mimi si mtaalamu wa kuunganisha link ningeziunganisha hapa.
Nina mtoto wa miaka mitano lakini hatukuweza kuwa pamoja na baba yake, na yeye ameoa mwishoni mwa mwaka jana.
Hatukuwa tumeoana na tulikuwa tukiishi kila mtu na kwake lakini hakuwahi kumtunza mtoto yaani namaanisha pesa ya matumizi. mtoto alipoanza shule tukawa tunatoa ada ya shule nusu kwa nusu wakati yeye ana kazi ya kumlipa mshahara mkubwa kuliko mimi. Kwa sasa analipa yote ila nayo kwa usumbufu sana na kulipa kwa mafungu mafungu. naongelea mtu anayelipywa zaidi ya milioni tatu mshahara kwa mwezi na biashara zingine za pembeni.
Mwaka jana mwanzoni akasema atakuwa anatoa elfu 40 kwa wiki ya matumizi yaani hiyo ikawa ni kwa mara ya kwanza, napo ikawa mpaka tukumbushane. Juzi kati hapa kaja na mpya kuwa anafungua account ya mtoto na atakuwa anaweka elfu 50 kwa mwezi kwahiyo hatoweza kutoa hela ya matumizi. Lakini cha kushangaza siku akimuhitaji mtoto atataka avalishwe vizuri apendeze asukwe vizuri na kadhalika. And he is very good at making promises kwa mtoto kuwa ntakununulia hiki nitakununulia hiki but kwenye simu ana kama miezi mitano hajamuona ni simu tu tena za usumbufu mana anaweza kukurupuka hata saa saba za usiku anataka kuongea na mtoto namwambia apige mchana. Kwa kweli leo nimeamka nina hasira sana sijui nimuweke kundi gani kwa kweli.Ndugu zake wanajua mambo yake na mara ya mwisho walinambia kama hataki kumtunza mtoto nimwache atakuja juta badae.
Hivi binadamu wa hivi nina deal nae vipi? Kwani jukumu la baba kama mzazi ni nini?