Jana tr. 13 Nov 13 nimetimiza miaka miwili iliyokamilika hapa Jamii forums .
Si haba kuufikisha umri huo , si pafupi sana , aidha si parefu sana , ni kama kati kwa kati .
Kwani wapo wengi nilio wakuta , na sasa hawapo tena.
Ktk msafara wa hadi kufika hapa nimeishaikwaa Ban 1 ya 14 days , ambapo niliichukulia kama ni sehemu ya ukomavu hivi , ama ni kama kijana wa kiume kupita jandoni , au wa kike kuzibuliwa bikira.
Kwa mapenzi mema nikiombacho kwenu ni mnitakie kheri na uzima niendelee kufurahia maisha ya humu Jf .
H. O . E
Thanks mrembo! Afu siku yangu kama hii , ungetinga hapa ukiwa hiyo mishedo umeiongezea mkolezo! Afu ukazinyanyua na hizo mboni mkabala , wahisani watathmini ! Hujachoka kuangalia chini ?