Jude Thadaeus Ruwa'ichi: Wakatoliki 'Feki' wapuuzwe, imani ya watu hao ni "feki" na haina mizizi

Jude Thadaeus Ruwa'ichi: Wakatoliki 'Feki' wapuuzwe, imani ya watu hao ni "feki" na haina mizizi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, amewatahadharisha walezi na wazazi kuwapuuza vijana wanaojigamba kuwa ni Wakristo huku wakikashifu kanisa, akieleza kuwa imani ya watu hao ni "feki" na haina mizizi.

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni katika Parokia ya Mtakatifu Gaspar-Mbezi Beach, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa ajili ya walezi wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu Jimbo. Kwa mujibu wa Gazeti Tumaini Letu, Askofu Ruwa'ichi amebainisha kuwa chimbuko la vijana hao kukashifu imani yao ni ukosefu wa misingi imara ya malezi tangu utotoni.

"Zama hizi za sasa wanajitokeza vijana na kujigamba wao ni Wakristo, lakini wamekuwa wakiuchimbia mwili na Ukristo wenyewe, japo kama ni kweli, kwanini wanauchimbia mwili na Ukristo? Na hao Ukristo wao ni 'feki', na hauna mizizi wala kina, alisema Askofu Mkuu Ruwa'ichi.

Askofu Mkuu amesisitiza kuwa malezi yaliyotengemaa yanahitaji uwepo wa wazazi wote wawili (mama na baba), kwani uwepo wa mzazi mmoja pekee unaweza kusababisha "ulemavu wa kiroho" katika ukuaji wa mtoto. Aidha, amewakumbusha walezi kuzingatia tofauti za kisaikolojia kati ya watoto wa kiume na wa kike tangu wakiwa wadogo.

Askofu Mkuu Ruwa'ichi alisema kwamba, malezi yaliyotengemaa yanamhitaji mama na baba, kwa sababu uwepo wa watu hao huleta hali nzuri ya kutengemaa, na kuwepo kwa mzazi mmoja kuna hatari kubwa ya kulemaa kwa familia.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ruwa'ichi, wanadamu wamejaliwa tunu mbalimbali, ambazo nyingine huitwa fadhila, japokuwa kuna maelekeo mengine yanaweza yakaitwa ni uovu au ulemavu.

Aliendelea kusema kwamba, kuna baadhi ya tunu zinaweza kusifiwa kama ni fadhila, ambazo ni upendo, urafiki, utu wema na huruma, japokuwa huwa haziji zenyewe, bali ni kwa sababu ya malezi bora.

Askofu huyo, aliwasisitiza walezi wafahamu kuwa, mtoto asipolelewa wala kurithishwa tunu zilizo bora, anakuwa mlemavu, japo siyo wa viungo bali ni wa roho, na anaweza kuumiza zaidi kuliko hata yule wa viungo.

Katika homilia yake, Askofu ameeleza kuwa fadhila kama upendo, urafiki, utu wema, na huruma haziji kwa bahati mbaya, bali ni matunda ya malezi bora.
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, amewatahadharisha walezi na wazazi kuwapuuza vijana wanaojigamba kuwa ni Wakristo huku wakikashifu kanisa, akieleza kuwa imani ya watu hao ni "feki" na haina mizizi.
Ni dalii wazi ya mwanzo wa mtengano wa makundi ndani ya katoliki. Kanisa katoliki halitakuwa the same again. Kitima kashalikoroga, ni wakati muafaka wa kungatuka kwa huyu Padre ili kulinusuru kanisa.
 
Ni dalii wazi ya mwanzo wa mtengano wa makundi ndani ya katoliki. Kanisa katoliki halitakuwa the same again. Kitima kashalikoroga, ni wakati muafaka wa kungatuka kwa huyu Padre ili kulinusuru kanisa.
unashabikia mambo kijuu kama ungefatilia historia ya kanisa katoliki ndilo lilizaa karibuni madhehebu yote makubwa ya dini ya kikiristo kuanzaia Lutheran, Anglican na mengineyo lakini halijawahi kutetereka bado linazidi kuwa imara.
Mnatengeneza wakatoliki feki halafu mnaenda kujipendekeza kwa Papa akili zenu sifuri ndio maana mlifeli form four
 
Ni dalii wazi ya mwanzo wa mtengano wa makundi ndani ya katoliki. Kanisa katoliki halitakuwa the same again. Kitima kashalikoroga, ni wakati muafaka wa kungatuka kwa huyu Padre ili kulinusuru kanisa.
Watu hawajaanza leo kujitenga na Kanisa na hao wanaoona Kanisa haliendi na wanavyotaka wao wana ruhsa ya kuondoka.
 
Ni dalii wazi ya mwanzo wa mtengano wa makundi ndani ya katoliki. Kanisa katoliki halitakuwa the same again. Kitima kashalikoroga, ni wakati muafaka wa kungatuka kwa huyu Padre ili kulinusuru kanisa.
images (30).jpeg
Leo nimeona kovu la jeraha jichoni limeshafutika.
 
Watu hawajaanza leo kujitenga na Kanisa na hao wanaoona Kanisa haliendi na wanavyotaka wao wana ruhsa ya kuondoka.
Ni kweli hawajaanza leo. Ila kuna uchafu na uchafu. Safari hii uchafu huu ni wa aina yake, tathmini tu hasara iliyojitokeza ndio utajua kuwa ya safari hii ni mpya. Hivyo hata mgawanyiko wake ni wa pekee si wa kulinganishwa na zile nyingine.
Mteteeni Kitima muendeleze madhara, kupanga ni kuchagua.
 
unashabikia mambo kijuu kama ungefatilia historia ya kanisa katoliki ndilo lilizaa karibuni madhehebu yote makubwa ya dini ya kikiristo kuanzaia Lutheran, Anglican na mengineyo lakini halijawahi kutetereka bado linazidi kuwa imara.
Mnatengeneza wakatoliki feki halafu mnaenda kujipendekeza kwa Papa akili zenu sifuri ndio maana mlifeli form four
"ungefatilia historia ya kanisa katoliki ndilo lilizaa karibuni madhehebu yote makubwa....." mwisho wa nukuu. Neno "LILIZAA" binafsi sikubaliani na tathmini hii. Katoliki haikuzaa hayo madhehebu mengine, bali ni watu waliojitenga toka katoliki kutokana na kutokubaliana kwa idiolojia ya katoliki. Yaani mtafaruku mkubwa ulitokea. sitoingia ndani katika historia.
Kusema kuwa CCM imezaa CHADEMA ni dhana potovu, ila ukisema Muasisi wa chadema "Mtei" na baadhi ya wanachadema wametokea CCM ni kweli. Hivyo usipoteshe watu.
 
Ni kweli hawajaanza leo. Ila kuna uchafu na uchafu. Safari hii uchafu huu ni wa aina yake, tathmini tu hasara iliyojitokeza ndio utajua kuwa ya safari hii ni mpya. Hivyo hata mgawanyiko wake ni wa pekee si wa kulinganishwa na zile nyingine.
Mteteeni Kitima muendeleze madhara, kupanga ni kuchagua.
Unajitekenya na kucheka mwenyewe. Eti mgawanyiko wa mamluki wa kukodiwa 20 ndiyo uende kuligawa Kanisa.

Kanisa Katoliki halijaanza leo kujadiliana ndani kwa ndani kuhusu "theolojia ya ukombozi". Hakuna jambo jipya hapo. Kama hamjui, hata Pope Leo XIV mliyeenda kumuona anasapoti "theolojia ya ukombozi"!

Hivi mliongozana na hao kina Lucy huko Vatican au mlipeleka tu zawadi za kinafki za kitabu cha Nyerere na kujichekeshachekesha?
 
Ukatoliki sio dini ni kikundi au kizungu Occult
Dini gani unatakiwa uwe na kitambulisho na na namba kukutambulisha wewe, na hata kwenye habari za kidunia wanaawatambua kama Catholic membership na sio waumini

Ndio maana huwa wanakataa kuzika wafu ambao wanaamini sio wanachama wao, halafu mnaiyta hii ni dini au ni kikundi cha wachawi?

1769952598126.png

1769952522702.png
 
Ni dalii wazi ya mwanzo wa mtengano wa makundi ndani ya katoliki. Kanisa katoliki halitakuwa the same again. Kitima kashalikoroga, ni wakati muafaka wa kungatuka kwa huyu Padre ili kulinusuru kanisa.
Kalikorogaje?

Au ndiyo mwendelezo wa ile vita?

Kukemea uovu wa watawala sasa umegeuzwa kuwa ni msamiati wa kulikoroga?
 
Kalikorogaje?

Au ndiyo mwendelezo wa ile vita?

Kukemea uovu wa watawala sasa umegeuzwa kuwa ni msamiati wa kulikoroga?
Hivi Kanisa likiamua kuachana na hayo mambo ya siasa kutatokea nini? Au kwakuwa Papa ana ubarozi wake hapa wa kiserikali ndiyo kunalilazimisha Kanisa kujiingiza kwenye mijadala ya kisiasa?

Nimeshaona hata Padre mmoja mzungu siyo mzaliwa wa Tanzania na siyo mtanzania lakini ni shabiki mkubwa sana wa siasa za Tanzania
 
Back
Top Bottom