Jua linapoelekea kuzama, Kinana utakumbukwa

Jua linapoelekea kuzama, Kinana utakumbukwa

pepsin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
3,486
Reaction score
6,172
Kati ya watu waliopambana kukemea uzembe wa CCM ni katibu mkuu wa CCM, bwana Kinana. Ukiacha kashfa ya meli yake kukutwa na nyara za serikali isivyo halali, yaani meno ya tembo, bado bwana huyu alihangaika sana kuiokoa CCM.

Alijaribu kila namna kujishusha na kushiriki na sisi watu wa hali ya nchi ili chama chake kiaminiwe tena lakini wenzake hawakumuunga mkono itoshavyo. Wakati yeye anahangaika huku chini,viongozi wenzake wanakwea ndege na kutembea aghaibuni bila kujali.

Ilifikia mahali akakemea utendaji mbovu wa viongozi wa serikali kutoka chama chake lakini aliishia kupuuzwa na kukejeliwa.

Sasa na yeye amekaa kimya, amekata tamaa na kufanya chama chake kikaribie kaburi la kisiasa kiurahisi zaidi.

Wana CCM wa kweli, mtamkumbuka sana mzee wenu huyu baada ya Oktoba. Alitaka sana kukisaidia chama lakini hamkumjali.Wakati yeye anashiriki na wananchi kwenye shughuli mbalimbali, hamna kiongozi yeyote kuanzia Taifa, mikoa, wilaya, tarafa, kata mpaka kijiji aliyemwelewa na kumuunga mkono.

Sasa jua la CCM linachoea, mtamkumbuka mzee Kinana sana.
 
Nakumbuka Kinana na Nape walivyomshauri mwenye mamlaka ya uteuzi wa mawaziri kuhusu mawazi mizigo. Mwenye mamlaka aliwabeza. Huo ukawa mwanzo wa wananchi kudhani kuwa mwenye mamlaka anaunga mkono utendaji mbovu wa mawaziri.
 
Hivi kinana yupo wapi na zile ngonjera za kubeba tofali, Kupalilia, Na maigizo mengine waliyokuwa wanayafanya maana hatumsikii au amesombwa na mafuriko ya Ukawa
 
Back
Top Bottom