Bonson
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 183
- 147
Mheshimiwa JPM,
Kwanza nianze kwa kukiri kwamba sina hofu na nia yako ya kutaka kuwainua wanyonge wa nchi hii. Pia sina shaka na msimamo wako wa kupinga ufisadi kwa vitendo. Jambo moja linalonipa shida ni lugha kali unayoitumia dhidi ya WAWEKEZAJI. Mheshimiwa, huna budi kukumbuka kwamba baadhi ya wawekezaji wametoa ajira kwa zaidi ya wanyonge 100; ina maana kwa hao wanyonge 100 kuna familia kubwa nyuma yao inayotegemea huo mshahara toka kwa mwekezaji. Kwa mfano tuu; endapo kila mfanyakazi anategemewa na watu angalau 4; ina maana muwekezaji anawawezesha watu zaidi ya 400. Hivyo basi, nakubaliana na jitihada ya kuwatetea WANYONGE, lakini usisahau tunahitaji MATAJIRI/WAWEKEZAJI zaidi ili amani iendelee na nchi iende mbele.
Tusijejikuta tunakuwa nchi inayochukia MATAJIRI na WAWEKEZAJI.
ASANTE
Mungu ibariki Tanzania.