mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,073
Naunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa kwa kasi kubwa na Mh. Rais na Serikari kwa ujumla.
Ndani ya kipindi kifupi ufufuko wa utendaji wenye nidhamu karibu katika idara,waizara na taasisi nyingi za umma umelejea..Lakini pia ufahamu wa wananchi juu ya mikono,miguu,kifua,sauti ya serikari kuzunguka maisha ya kila siku umehimalika mno pasipo kusahau hofu kuu waliopata wafuja mali,mafisadi ,wapiga dili na watumia madaraka vibaya.
Angalizo hili linahusu baadhi ya maagizo na utekelezaji wa baadhi ya hatua kiserikari zenye harufu ya kugombanisha serikari na mabosi wake{wananchi -Maskini,malofa,wanyonge,matajiri,wajinga,werevu,wacha Mungu hata wapagani} zinazosimamiwa na kuratibiwa na wateule wa Mh. Rais wenye kiu na walioonyesha kiu,shauku na njaa ya kuyataka madaraka makuu kisiasa hasa uraisi wa JMT..
Kutukuka kwa kila utendalo msingi wake ni wananchi kuishi maisha ya furaha,ustawi,uendelevu,matumaini chanya n.k. Ikiwa wananchi walio wengi {maelfu kwa maelfu} tena maskini wataishi kwa hofu na kukata tamaa kwa sababu ya utekelezaji wa mikakati isiotoa masuruhisho ya kudumu juu ya sababu zilizopelekea utekelezaji wake nachelea kusema vilio , mateso na mahangaiko ya wahanga yaweza sababisha mengi mazuri kuoneka mabaya na mabaya kuonekana mazuri..hata yamkini wazuri kuonekana wabaya na wabaya kuonekana wazuri.
Hakuna Serikari bila wananchi ila wananchi waweza kuwepo bila uwepo wa serikari..Vema hekima ikahusishwa sana katika utekelezaji wa mipango,mikakati ,maazimio na maagizo yanayogusa maisha ya wananchi kwa kiwango kikubwa .
Baadhi ya viongozi wa kisiasa wenye kiu ya kupanda ngazi za kimadaraka kila watendalo/wasemalo yamkini likawa na lengo la kujijenga {Nafsi zao,nia zao binafsi,matamanio yao binafsi ,kiu zao binafsi,mipango yao binafsi} kimkakati kwa malengo ya huko mbeleni kupitia mgongo wa HAPA KAZI TU..sitoshangaa kuona wakitekeleza yasiotekeleza ili kuharibu sura njema ya mapambano ya dhati toka His Excellence JPM na serikari ya awamu ya 5.
Udhibiti wa kina unapaswa kuwepo..uhakiki wa mapana