Hapo ndo wabongo tunapozingua, tumekalia majungu tu na kuponda kila kitu,,
Hata kama ana mapungufu yake joyce kiria ni mfano, kwa elimu ya msingi kufika levo aliyonayo lazima tumpe credit kwa hiko anatisha, tuna watu wangapi mitahani wana masters na elimu zinginezo hawaeleweki, wameshindwa kubuni hata biashara ya pipi,, mwenzetu anatengeneza pesa tunampiga majungu hana shule mara hawezi kuwa oprah sijui tyra banks wakati ukweli tunaujua moyoni
Joyce kiria amezaliwa kijijini huko moshi tena kwenye familia duni, mjini kaja kama house girl lakini after 10 years in town amepanda kutoka u house girl mpaka tv host mkubwa kibongo bongo,,,wakati kuna mijitu imezaliwa town hapa, inatoka familia nzuri na imekaa town zaidi ya 30 years, ina elimu ya kutosha sijui udsm, mzumbe, oxford, etc lakini haina chochote imekalia kulalamikia ccm tu badala ya kujituma kumake things happen...
Sasa assume joyce ndo angezaliwa familia mambo safi ingempeleka shule angekuwa wapi sasa hivi
Kumfananisha na oprah ni ujinga as oprah amezaliwa Atlanta USA wakati joyce amezaliwa Kishumundu kivipi watakuwa sawa?
Tukatae tukubali oprah was born at a right place in a right time while joyce is born at a wrong place in a right time ( nimesema right time sabab tv show zimemkuta katika umri sahihi)
Mtakalia hivyo hivyo kumponda joyce wakati sasa hivi wanawake live inarushwa kwenye dstv through africa magic swahili na inaangaliwa na Africa nzima,, unafikiri anaingiza bei gani?