Josephine Lemoyan na Pamela Maasay wachaguliwa kuwa wabunge wa Afrika Mashariki kutoka CHADEMA

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,279
Baada ya Wabunge watengua kanuni kuruhusu Bunge kurejea leo saa 10 jioni badala ya 11 kuruhusu uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Chadema .
Tutakuletea yanayojiri kutoka Bungeni kwenye uchaguzi huo.
Wagombea waliteuliwa na Chadema kugombea ubunge wa Afrika Mashariki EALA.

1. Profesa Abdalla Safari
2. Salum Mwalim
3. Ezekia Wenje
4. Josephine Lemoyan
5. Lawrence Masha
6. Pamela Massay

========

UPDATES

=======

Sababu za kuzuia Uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki EALA kurushwa live mpaka hazijajulikana.

Bungeni bado uchaguzi wa ubunge wa EALA haujaanza Bado bunge la kawaida linaendelea.
[HASHTAG]#BUNGENI[/HASHTAG] Wapo wabunge wengine humu wanajifanya wanajua kimombo kumbe hakuna kitu - Spika wa Bunge, Job Ndugai
Professa Abdallah Jumbe Safari amemaliza kujinadi mbele ya Wabunge
Josephine Lemoyan amesema anamini kuwa uzoefu wake katika taaluma ya elimu ya jamii utamsaidia kufikisha malengo mbalimbali yaliyowekwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Ezekiel Wenje anajinadi sasa mbele ya wabunge .
Lawrence Kego Masha anajinadai sasa mbele ya wabunge.
Lawrence Masha amesema yeye ni mzalendo na kwamba ataendelea uzalendo huo kutetea maslahi ya Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki.
Pamela Simon Maasay anajinadi sasa mbele ya wabunge.
Mgombea wa uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kwa upande wa Chadema, Salum Mwalimu ametumia jina la Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kujinadi.

Wakati akihitimisha maombi yake ya kura baada ya kuulizwa maswali matatu na wabunge, Mwalimu amesema atakapovuka mpaka wa Tanzania kuiwakilisha katika mataifa mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki endapo atachaguliwa atakuwa mwakilishi wa Taifa na si chama.
Zoezi la upigaji kura linaendelea sasa katika ukumbi wa Bunge ili kuchagua wabunge wawili wa CHADEMA watakaowaikilisha [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] EALA.
tmp_31856-IMG_20170510_200930-260824995.jpg

Bunge limerudi hewani na liko LIVE sasa. Fuatilia moja kwa moja hapo chini;

Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea muda huu bungeni.
Wabunge wa CHADEMA waliochaguliwa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
============
Matokeo ya uchaguzi kura kwa wagombea nafasi za ubunge wa Afrika Mashariki EALA.
dallah Safari kura 35.
2-Wenje kura 34
3-Lawrence Masha kura 44
4-Salim Mwalimu kura 54
5- Josephine Lemoyan kura 219
6-Pamela Maasay kura 200.
Washindi waliochaguliwa na wabunge.
1-Pamela Maasay
2-Josephine Lemoyan

1. Josephine Lemoyan
2. Pamela Maasay

Wabunge: 9
Wanaume: 4
Wanawake 5


IMG_20170510_220912.jpg

FB_IMG_1494446883632.jpg

Pamela Maasay
FB_IMG_1494447124727.jpg

Josephine Lemoyan

========

Matokeo:

Kura zilizopigwa 296, Kura halali 296 .Abdallah Safari 35,

Wenje 34,

Josephine Lemoyan 219,

Lawrence Masha 44,

Pamela Maasay 200 na Salim Mwalimu 54

Hivyo, Jesephine Lemoyan na Pamela Maasay ndio wabunge wa EALA rasmi.
 
Chadema wamekubali kucheza Ngoma ya CCM.... Kulikuwa hakuna namna kuliwabidi, ila tutaangalia ni namna gani wataicheza, kwa Werevu au itakuwa ni kama CCM watakavyo.
 
Kumbe hawakwenda mahakamani.
Ilipaswa wapigwe hata faini au onyo kama wanafanya leo kile walichotakiwa kufanya siku nyingi zilizopita.
Hii ni ishara chama hakithamini MUDA
 
Vipi ule Mpango wa Mwansheria na Wakili Msomi Mh. Tundu Lissu kupinga Mahakamani Mchakato wa Uchaguzi wote kuanzia Mwanzo Kama alivyoahidi kwa Madai eti ni Batili?
 
Sisi huku mtaani, tunawasikia wanasema walikuwa sahihi kuleta watu wawili, na wataenda mahakamani. Leo kukubali wanachokifanya ni Upotevu wa Muda, ilipaswa wafanye hili wanachofanya leo walipaswa kufanya kabla ya uchaguzi wa mwanzo. Wakibadilisha misimamo ni vizuri kuutangazia umma pia
Unajua, hawa jamaa kimsingi wamevurugwa na kwa kuwa wamezoea sana mahakamani, ndo maana kila kitu wao na mahakama, kanuni za bunge watunge wao alafu wakishindana bungeni eti wanakwenda mahakamani, lakini hawa watz hawatoendelea kuwa mazoba kama wafikiriavyo wao- tumechoka na maamuzi yao ya kukurupuka
 
Hakuna mwaka ambao ccm iliwahi kuwa na dhamira njema na nchi hii .

Mbona Chadema ilipeleka Mgombea wa Ubunge 2015 Kigoma Mjini ili Mgombea wa CCM wa Darsa la Saba ashinde kwa kuwa kura A Wapinzani zingegawanyika ili kumkomoa Zitto Kabwe?

Mmesahau mlivyomkomesha Julius Mtatiro kule Segerea mpaka CCM ikashinda na Yule aligawanya kura mkampa Ubunge wa Viti Maalum Kama zawadi?

Msitudanganye na kuzuga mambo ya Uzalendo mnapozidiwa Maarifa na CCM
 
Unajua, hawa jamaa kimsingi wamevurugwa na kwa kuwa wamezoea sana mahakamani, ndo maana kila kitu wao na mahakama, kanuni za bunge watunge wao alafu wakishindana bungeni eti wanakwenda mahakamani, lakini hawa watz hawatoendelea kuwa mazoba kama wafikiriavyo wao- tumechoka na maamuzi yao ya kukurupuka
Mkuu sema nimechoka, usitusemee na sisi wengine ambao hatuko kwenye moyo wako
 
Back
Top Bottom