Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MWILI wa aliyekua Mwandishi wa habari Josephat Isango unatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne, saa nne asubuhi nyumbani kwao Kisasida mkoani Singida.
Marehemu Isango alifariki dunia jana mapema asubuhi katika hospitali ya Ikungi mkoani Singida ambapo alilazwa kwa wiki mbili akisumbuliwa na Kifua, hata hivyo uchunguzi wa afaya yake ul;ibainisha ana tatizo la kupanuka kwa moyo.
Enzi za uhai wake, Marehemu alifanya kazi katika kampuni mbalimbali ikiwemo Free Media wazalishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari pia aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya Hali Halisi Publishers wazalishaji wa magazeti ya Mawio na MwanaHALISI.
Mwandishi huyo ambaye alisifika kwa ujasili wake katika kutetea haki za wanyonge, Mwaka 2015 aliwahi kukumbwa na tukio la kushambuliwa na polisi wa FFU eneo la mbele ya makao makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jijini Dar es Salaam alipokuwa na waandishi wengine wakisubiri kuwasili kwa viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Aliwahi kuugua akiwa jijini Dar es Salaam na baada ya muda mfupi aliamua kusafiri kwenda Singida, mkoa wa nyumbani kwao ndipo mauti yakamkuta.