Joseph Yona: Iwapo nikichaguliwa kuwa spika, manifesto yangu hii hapa -- mambo 14

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
IWAPO MIMI #JOSEPH #YONA NIKICHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE LETU TUKUFU.....MANIFESTO YANGU MAMBO 14

Iwapo nikiukosa Uspika wa Bunge letu tukufu, Naibu Spika #Tulia #Ackson Naibu SPIKA Anafaa kuwa Spika kama amechukua Fomu, Ana nidhamu na Taifa na Mkuu wa nchi.


MANIFESTO YANGU MAMBO 14.

(1).Ningetambua majukumu ya bunge Letu tukufu kuwa ni kuisimamia serikali, kuishauri serikali, Kutunga Sheria na kutambua kuwa bunge ni Muhimili ambao unatambua pamoja kuwa Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ni Mkuu wa nchi, hivyo nguvu yake haiwezi kulinganishwa na Mihimili mingine lazima kumshauri kwa nidhamu. Na pia ni marufuku kwa mbunge yeyote kumuongelea Rais kwa dhihaka au kashfa, Mbunge yeyote akitaka kumuongelea Rais lazima aongee kwa nidhamu na Heshima.

(2) Ningepunguza Posho za wabunge kwa 50% na mishahara yao Ningeipunguza kwa 50%.

(3) Mikopo ya wabunge nayo Ningeipunguza kwa 50%.

(4) Mafao yao ya kustaafu nayo yangepungua kwa 50%.

(5) Ningepiga Marufuku kuongea bungeni kwa mihemko, kutafuta sifa, au matusi ningeweka Sheria kali za wanaosaka sifa.

(6) Bunge linatakiwa kuwa Kazini kwa Mbunge, hivyo ni marufuku kwa mbunge kuchelewa kufika au kuwahi kutoka bungeni, ningeweka Sheria kali.

(7) Mbunge anatakiwa awepo Bungeni muda woote labda kama ni mgonjwa au umepata ruksa maalum kutoka kwa Naibu Spika.

(8).Wale wabunge 19 wa Chadema na wale wa kuchaguliwa wa vyama vya upinzani, ningewafanya wawe kambi ya upinzani bungeni, na ningewapa nguvu kukishauri chama tawala kwa nidhamu, ningebadili sheria ya kutoa kambi ya upinzani bungeni, hata mpinzani akiwa mmoja ataunda kambi ya upinzani.

(9) Ukimtukana Spika wa bunge au naibu spika au Mbunge yeyote adhabu ni ubunge unakoma hapo hapo, hatutaki wahuni Bunge tukufu.

(10). Ikitokea mbunge kafariki, kajiuzulu au vyovyote vile basi ofisi ya Bunge itakitaarifu chama chake kiteue mbunge mwingine wa kumalizia kipindi kilichobaki, hapa nitapigania sheria ibadilishwe ili tupunguze magharama ya kurudia uchaguzi.

(11) Ni marufuku mbunge kutibiwa nje ya nchi, Mbunge akiugua awahi kwenye Hospitali na vituo vya afya wanavyovisifia, na utaratibu utakaotumika kwa wabunge ni utaratibu wa bima ya afya.

(12) Ubunge utakuwa wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano tu, kama Rais.

(13) Baada ya vipindi vya bunge kumalizika wabunge watatakiwa warudi majimboni, ili kusikiliza kero na kuzirejesha ofisi ya katibu wa bunge pindi bunge jipya lifikapo na nakala ya kopy ya kero ifike ofisi ya katibu Mkuu wa chama chako.

(14) Ni marufuku kwa mbunge yeyote kumuongelea mtu yeyote ambaye hayupo bungeni, hivyo hoja za mbunge lazima zijikite kwenye kutatua kero, mijadala ya kushughulikia shida za wananchi basi.

IMG_20220114_145724_115.jpg
 
Ukishiba manifesto ubadilika.

Viongozi wa kiafrica huwa na akili wakishatoka madarakani.

Upinga katiba mpya wakiwa madarakani uiunga mkono mfumo wa kutoa maamuzi ukiwatupa
 
Bora umeweka ugoro wako hadharani na kujiondoa mapema ili huko mbele watu wawe na reference yako iwe rahisi kukutupa nje ya wigo, kwa hiki ulichoandika hakuna mbunge atakupa kura.

StStrategic plan huwa zinafanywa baaada ya kuingia kwenye fahari na si kabla, hakuna binadamu unayemwambia nikiwa boss wako nakuondolea chai na boflo alafu akakupa ushirikiano, NO!
 
Back
Top Bottom