Joseph Msukuma amkimbia Alphonce Mawazo ITV

Joseph Msukuma amkimbia Alphonce Mawazo ITV

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
235
Reaction score
1,275
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita bw Joseph Msukuma amemkimbia kamanda Alphonce Mawazo Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa wa Geita katika kipindi cha Mzalendo kinachorushwa na stesheni ya ITV Leo tarehe 18/09/2014 saa 1:30.

Kutokana na uwezo mdogo wa kujenga hoja wa mwenyekiti huyo ameamua kutoa taarifa ya udhuru baada ya kusikia atakuwa na Alphonce Mawazo kwenye kipindi.

Kwa hili linaonyesha kuwa CCM kuwa na viongozi ambao wana uwezo wa kujenga hoja kwenye vipindi mbalimbali na midaaro kama utakummbuka uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo viongozi wa CCM walikatazwa kuingia kwenye midaharo na aliekuwa katibu mkuu bw Yusuph Makamba baada ya kuona uwezo mdogo wa wanaccm waliogombea ubunge wakati ule.

Kutokana na hali hiyo imelazimika waandishi wa habari kumtafuta mwenyekiti wa CUF mkoa wa Dar es salaam kuchukua nafasi ya msukuma.

Naomba kuwasilisha hoja.
 
wapo wana CCM wenzangu wenye uwezo mzuri tu wa kujenga hoja tatizo hawana cha kutoa kwa wapiga kura ila wapo watu wazuri sana ndo sababu nauliza tangu juzi kuwa pesa tuliyokodisha chama haijaisha ili chama kirudi mikononi mwa wanachama na je miaka tuliyokodisha haijaisha CCM yangu kwanini unadhalilishwa ivi na hawa wapangaji?
 
Huyu bwana namjua sana hajui kusoma wala kuandika ndio kibajaji anawatetea kwenye katiba
 
Kawaida ya CCM hakuna anayeweza kumudu debates kwenye TV, kuanzia viongozi wao kitaifa hadi mabalozi wa nyumba 10.
 
Hizi sasa ni dharau Msukuma na Mawazo wapi na wapi?Msukuma mburula mno.
 
WABHEJASANA;
Hapana umeongopa kusoma anajua na kuandika pia sema hana elimu ya zaidiya darasa la saba.

Mkoa wa Geita ccm inaongozwa na vilaza waliofeli sijui kwann? eti WABHEJASANA hebu nisaidie ni kwa nn?
Msukuma-M/kiti wa mkoa~la saba failure
Mhoja Mapande-M/kiti wa wilaya Geita Mji~la saba failure!
Katibu naye ni la 7,
 
Last edited by a moderator:
Ccm haina viongozi wenye maono,hawako tayari kukumbana na mawazo kinzani,wameingia serikalini au kwenye chama kwa lengo la maslahi.
Hawawezi kujenga hoja,sana sana watatoa vitisho,na kusena watakuitia polisi.Msukuma anajua angeumbuka maana anajua hadi kupata cheo hicho alikipataje
 
Nikweli anajua kusoma na kuandika tusimchafue kwa hilo, ila unajua kuwa sehemu ya mali aliyonayo ni ya mzee wa CHATO?

Ndio maana nimesema alikimbia kunusuru mzee wa chato,ambaye viwanja na majumba aliyonayo acha kabisa!
 
CCM imebaki kama gofu!!!walioko ndani ni popo na bundi ambao wote hutoka usiku!!!!
 
Toka lini uwezo wa kujenga hoja ndo sifa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi CCM? Walikatazwa kushiriki midahalo,hata Kikwete naye alikatzwa ,kwani wanajuana walivyopatikana. Sifa ya CCM kuwa kiongozi ni ufisadi,kuwanunulia pilau,usafiri wa malori kuwasafirisha kwenye mikutano,hatimaye kuwapa posho. Wanategemea polis I/dola kubaki madarakani
 
kamanda alphonce mawazo anajua vizuri maisha ya wananchi vijijini amezunguka kanda zote anauthibitisho anachokisimamia
amechanja mbuga vijijini na mji midogo kwahiyo msukuma ni haki yake kumkimbia asije akaumbuka
ccm hawana lakutudaganya.
 
Back
Top Bottom