Joseph Mbilinyi aka Sugu aitangaza Fiesta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Mbilinyi aka Sugu aitangaza Fiesta

Discussion in 'Entertainment' started by Gamba Jipya, Jul 8, 2011.

 1. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zilizo nifikia hivi punde ni kuwa,
  Kama ilivyotarajiwa hatimaye mbunge wa mbeya mjini kwa tiketi ya CDM bwana Sugu sasa ameanza kampeni rasmi ya kulisifia na kulitangaza tamasha la Fiesta tofauti na alivyokuwa analipinga siku chache zilizopita, siku nzima ya leo sugu amekuwa anarushwa kwenye matangazo kadhaa akiipa sifa fiesta na kuwaahidi washabiki wa fiesta kuwa baada ya muda mrefu bila yeye kuperfom kwenye fiesta sasa wakati umewadia.

  Hii ndiyo misimamo ya wanasiasa wa CDM.
   
 2. chairman mao

  chairman mao Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeiona ile video anayoizungumzia fiesta na inaonekana kama si ya mwaka huu
   
 3. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, wanachofanya Clouds ni uhuni, nakumbuka Sugu aliwahi kuongea na hawa jamaa kuhusu fiesta ya mwaka 2007 akiwa USA, na ndiyo sauti wanayotumia leo kutangazia wakazi wa mbeya..... Pia wamechukua sauti ya Mwenyekiti wa chadema mkoa wa mbeya akiwasihi wananchi wajitokeze kesho.... Hii yote ni kampeni ya kutaka wakazi wa Mbeya wauzurie kwenye hilo onyesho ambalo Sugu alisema hatafanya kila njia lisifanyeke kwenye mkoa wake wa Mbeya.....

  Hii ni vita nyingine kati ya Sugu na Jamaa wa Cloudsfm, nadhani Sugu anaweza kuwafungulia kesi hawajamaa kwa kutumia sauti yake kwa maslahi ya kujinufaisha wao pasipo kumshirikisha.
   
 4. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ngoja tuone.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  hawa clouds wana uchokozi sana na wana mambo ya kitoto if this is the case: Hata leo kipindi cha Power Breakfast, PJ kanisononesha sana eti anaringanisha sauti za wabunge wa CDM kama vyura the way wanavyolalamika bungeni bila mpangilio.

  Kweli CCM inawalipa watu wengi sana.
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Nimeisoma katiba na manifesto ya CHADEMA hakuna neno FIESTA.......kwa hiyo huo ni msimamo wake Sugu kama ni kweli amesema
   
 7. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu. Toka asubuhi nilipo msikia jamaa aliyejitambulisha kama sijui mwenyetiki wa CHADEMA mkoa wa Mbeya kama sijakoseha cheo alichojitambulisha naocho, hapo ndipo nilipatwa na hofu na kujiuliza mwenyewe inakuwaje hii kitu ifanywe hivi ingali ili swala linajulikana kabisa juu ya utata wa Sugu na hawa jamaa... Kwenye mida ya mchana hivi nikasikia sauti ya Sugu ya miaka ya nyuma ikizungumzia fiesta ndipo nilipata picha kamili juu ya uhuni wa hawa jamaa wa CloudsFM
   
 8. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ni kwamba Sugu hajuazungumza chochote kuhusu FIESTA kwa kipindi hiki, zaidi cloudfm wamechukua sauti yake ya kipindi cha nyuma wakati akizungumzia FIESTA, na ndio wanaitumia leo kuwahamasisha wakazi wa Mbeya.
   
 9. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimeagiza bwana mdogo alirecord hilo tangazo mapema, nimelisikia leo clouds majira ya saa saba.
   
 10. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sheria imekaa vizuri sana juu ya hii issue, halafu uzuri kwenye background wameweka ile promo ya fiesta 2011. Tia mahakamani hawa jamaa mapema sana.
   
 11. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huu utata umekaaje hii na mimi naliskia hili tangazo????????????????????????????????
   
 12. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mahakama Ni wafuasi wa MAGAMBA, na washtakiwa ni wana MAGAMBA, nadhani ilii swala ni kubwa mno na nina wasi wasi haya mambo ya kawa makubwa na kufikia kuleta umarekani (Kupigana shaba tu hakuna cha zaidi hapo )
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni sugu ndiye aliyerekodi, kama siye angeshakanusha
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mh! Avatar yako inanitisha mnoo badilisha bana khaaaaaaaa
   
 15. opwa

  opwa Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni uongo mtupu, hizo nyimbo zimechakachuliwa. sugu kamwe hawezi kujihujum alichotangaza ni kampeni zake maeneo mawili na show ya muzik siku ya jmos viwanja vya luanda nzovwe. ingia kwa profile yake facebook kaweka hilo tangazo jana ucku
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimeongea na mtu kutoka Mbeya ameniambia kwamba kesho kutakuwa na burudani mbili. Fiest katika uwanja wa Sokoine kiingilio 3000 na Onesshe lingine litatumbuizwa na wakongwe kama Sugu,Mkoloni,Gsolo , Mchii mox na wengine katika viwanja vya shule ya msingi Rwanga Nzovwe kiingilio ni bure
   
 17. M

  Mibaso Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikweli kabisa kesho kuna show mbili yani fiesta ya sokoine ambayo itaanza sa 5 asubui mpaka sa 12 jion af na sho aloanda mh Sugu ya buure kabisa wakiwemo akina Adili mapacha soggy sugu mwenyewe mox nawengineo kwa mujibu wa radio moja hapa jijin show inaanza saa 4 asubui mpaka saa 6 usiku.
   
Loading...