Jose Mourinho tunayo leo na kesho

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
964
1,689
Alipohojiwa gwiji wa soka la Uholanzi na Mkufunzi wa soka Frank De Boer juu ya Jose Mourinho na Manchester United, De Boer aliponda kuwa wachezaji wazuri kama Marcus Rashford hawana cha kujifunza kwa Kocha huyo

Waandishi kama iliyo ada walimpa kashfa hiyo Jose, nae akasema tu "Jana nilisoma sehemu kuhusiana na Kocha mbovu zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Premier League, mpaka sasa ana mechi saba, ushindi sifuri na goli sifuri"

"Nafikiri Rashford ana mengi ya kujifunza kwangu Mshindi kuliko yeye mtu aliefeli" alimaliza Jose Mourinho na kisha akasimama na kuondoka zake, ni sehemu ya Maisha yake na ni sehemu ya utaratibu wake juu ya soka lake

Miaka yote na siku zote ameishi kwenye maisha ya kuamini zaidi misimamo yake isiyopindishwa, wakati anaondoka Chelsea kwa mara ya kwanza Mashabiki na wachezaji wakati wanaumia sana yeye aliwaambia Mourinho hajafa, Mourinho bado Kijana, bado ana muda mwingi wa kuzaliwa tena na kutenda tena maajabu

Alichosema bado hakikueleweka kirahisi lakini baada ya kupewa kazi ya Ukocha Inter Milan ndipo dunia ikaelewa maana ya maneno yale, inasemekana Mourinho anatumia sana mbinu za gwiji Helenio Herrera Kocha wa zamani wa Atletico Madrid ndizo alizoenda kutumia pale Inter Milan

Yalitokea mabadiliko makubwa sana kwenye kikosi cha Inter Milan, Waitaliano hawakumuelewa nini anataka kufanya ila mbele ya Waandishi aliwaambia, "samahani kwenu nyote mnaoumizwa na hiki ila vumilieni tupo kwenye Mapinduzi"

Walichoka zaidi pale ambapo Zlatan Ibrahimovic anaondoka Inter kuelekea Barcelona na Samuel Etoo anatoka Barca kwenda Inter, Jose alisema "Huu ni usajili mkubwa kuliko wa Cristiano Ronaldo, Ricardo Kaka kwangu Etoo ni usajili mkubwa zaidi ya hao wote hapo"

Hakueleweka pale ile Jose alitwaa Ubingwa wa Ulaya na Serie A akiwa na Etoo, aliondoka na Treble msimu ule kisha akasepa zake Real Madrid

Some people call me arrogant, but am European Champion and I think am the SPECIAL ONE
IMG_20210129_175902_141.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom