Jomeke na Siri za watu vijiweni

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Kuna Bwana mmoja maarufu anaitwa JOMEKE; Huyu bwana ni katika wale watu wasiokuwa na vifua, hana stahimala akiona jambo. Vijana wanasema friji lake haligandishi. Jomeke hawezi kabisa kuficha siri, akiskia jambo au akiona jambo hawezi kuvumilia lazima aseme

Sasa siku moja Jomeke kwenye kupitapita kwake akawafuma watu kichakani wanafanya mambo yao, basi wale jamaa kwakuwa wanamjua Jomeke na tabia zake wakaona leo tumekwisha, wakamwambia tafadhali haya yaishie hapa hapa usimwambie mtu, tutakupa chochote unachotaka ili ukae kimya.

Jomeke pia hakuwa mtu mwenye uwezo, alikuwa ni mtu mwenye uwezo ni mtu ana njaa zake zimejaa tele. Basi wale waliofumwa wakampa JOMEKE laki tatu ili akae kimya. Basi Jomeke akizichukua zile pesa huku shingo upande maana yeye hapendi kuonekana hana taarifa za watu.

Basi zikapita Kama siku 5 hivi Jomeke koo linamuwasha na kifua kinataka kupasuka lakini akifikiria zile pesa anavumilia. Siku ya sita akaenda kwenye kijiwe cha kahawa na kama unavyojua kwenye kijiwe cha kahawa kuna story yake lakini Jomeke hana la kusema hakuwa na story mpya.

Katika kile kijiwe cha kahawa na yule bwana aliyefumwa vichakani alikuwepo akimuangalia usoni Jomeke anavyohangaika. Kijiwe kimepamba moto kila anasema story yake.

Basi bwana Jomeke akaona isiwe shida, akasimama akanyamazisha watu wote kuongea, akaingiza mkono kwenye koti lake akatoa zile laki tatu akamwambia yule jamaa aliyemkuta vichakani. Bwana Pandu mie siwezi tena kuvumilia chukua laki tatu zako mie lazima na mie niseme

Jomeke kwa kujijuwa kumbe aliweza kuvumilia kutotumia pesa zile alizopewa maana alijijua kifua kitapasuka. Jomeke akatoa pesa akamshikisha mkononi yule bwana pesa zake “pesa zako hizi” akayamwaga yote mkahawani

Je, Kichwani mwako hapo una JOMEKE wako unaemjua?


Funzo:
Kuwa makini na mambo yako unayoyafanya kwani tunazungukwa na kina JOMEKE wengi sana katika maisha yetu na wengine siyo kwamba wanayatafuta bali taarifa zetu za siri tunawapelekea mwenyewe na baadae kutumaliza kabisa. JOMEKE hana dhamana atakuuza tu.​
 
Maboda boda wote ni ma jomeke.

Unaeza ukamkodi akupeleke sehemu, mkifika haondoki mpaka aone unaingia wapi au unakutana na nani.

Mie huwaga najiongekesha kwenye simu mpaka aondoke, basi unakuta ana zuga zuga kutengeneza boda yake kumbe hana la maana.
 
aisee ! Umenena vyema hao jamaa tabia zao zinafanana..
 
Kuna mdada anasema ana mimba yangu...
Yaan mpaka sasa furaha sina jamni daaah sijui nafanyaje hapa...
 
Huyo JOMEKE ni mimi kabisa .
 
Uko sahihi
 
Hili jina la JOMEKE limenifanya nione hii kama ni CODE , je who is JOMEKE in real life? 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…