John Rafael Boko angeandaliwa hata mchezo wa Kumuaga rasmi

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Ntaziita tetesi kwamba Azam Fc wameachana na Mchezaji wao John Boko Rafaeli,Akiwa ni kati ya wachezaji walioifikisha Azam hapo ilipo kwani kuanzia ligi daraja la kwanza mpaka Azam wanapanda ligi kuu yupo na wala hajawahi kwenda Timu nyingine na kurudi zaidi ya Azam fc.

Kama kweli Azam fc wameachana na Kijana Rafaeli Boko kwa njia za kienyeji sio sawa amewapa heshima na amecheza kwa kujituma sijawahi msikia katika Skendo yoyoye nje na ndani ya uwanja,wenzetu Ulaya mchezaji yeyote aliyecheza kwenye timu kwa muda mrefu huandaliwa mchezo wa heshima kwa kukubali mchango wake.

Kwa heri John Rafaeli Boko Mafanikio mema popote uendapo.
 
Sawa mkuu, ni vyema lakini akaandaliwa mechi yake ya mwisho..ingependeza sana
 
Bongo hatuna appreciation hata kidogo,unakumbuka ya maximo?mwishowe akatupiwa virago.so Boko anaweza akaachwa kienyeji Tu na life ikaendelea
 
Ila kweli huyu jamaa ni nembo ya Azam nitashangaa kama ataondoka kienyeji,lakini pia nitashangaa kama ataondoka Azam na kwenda timu nyingine ya hapa bongo kwani anakosa nini Azam?!
 
Nasikia jamaa alikataa kupunguza mshahara kama utaratibu mpya wa timu ya azam katika kubana matumizi.
 
Ila kweli huyu jamaa ni nembo ya Azam nitashangaa kama ataondoka kienyeji,lakini pia nitashangaa kama ataondoka Azam na kwenda timu nyingine ya hapa bongo kwani anakosa nini Azam?!
Hiyo kauli yako ndio imeifanya Azam ifanye vibaya misimu kibao kwa kulea lea amateur players

Makocha wawili tofauti mfululizo wanamkata bocco kwenye mipango yao this time akubali tu haiwezekani kila kocha anayekuja anamkata

Kwa uwekezaji wa Azam na aina ya wachezaji waliokuwa nao ni aibu ni time ya kufumua na kufanya transition ,kulea lea ndio imeifanya Azam iwe mbovu..na sio Bocco tu wapo wengi tu pale magalasa yaondolewe
 
hebu nipe takwimu za Boko wa Azam kafunga goli ngapi,Kacheza miaka mingapi,kafunga magoli muhimu mangapi buddy??
 
hebu nipe takwimu za Boko wa Azam kafunga goli ngapi,Kacheza miaka mingapi,kafunga magoli muhimu mangapi buddy??
Hao nao waache. Unafiki angekuwa ana staff soka hapo sawa wangeweza kumuandalia mechi, kuhama timu uandaliwe mechi ya heshima?!!
 
Back
Top Bottom