pole nyingi sana wafiwa , ukiacha makosa ya kibinadamu , hakika Nyerere alikuwa mzalendo halisi , mpaka leo familia yake inatibiwa Muhimbili , bali mafisadi wengi wa chama alichokianzisha hutibiwa INDIA , ULAYA NA AMERICA .
Mbowe,Mrema,Lipumba.SEIF shariff hamad,na viongozi wa kibao wa upinzani wanatibiwa nje ya nchi wote nao mafisadi kwa gharama za serikali nao mafisadi? Au hujui kuwa huwa wanaenda nje kutibiwa na kupima afya zao?
Nilimuuliza Butiku kuhusu Yericko. Butiku akasema nipe namba yake ya simu,nitamtafuta. Nilimpa Butiku hiyo namba. Sijui jambo gani lilitokea. Lakini baadaye Yericko akasema kwamba yeye hayupo katika familia ya Nyerere. Anajiita Nyerere kwa ajili babu yake mhehe alikuwa anaitwa Nyerere.
Mwana jf mwenzetu Andrew, poleni sana kwa msiba huu mkubwa na nadhani ndio wa kwanza kwa mtoto wa Mwalimu!.
Kusema ukweli baadhi ya wanafamilia wa Baba wa Taifa wako too low profile kiasi licha ya mimi kukulia jirani na Pale Msasani huku tukisoma darasa moja na Milton sikuwahi kusikia lolote kumhusu John zaidi ya kusikia alikuwa na cheo cha Capt. wa JWTZ na alikuwa ni fighter pilot wa Jet.