John Mnyika ana kwa ana na wananchi

John Mnyika ana kwa ana na wananchi

kidonge ki1

Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
15
Reaction score
3
Majira ya saa kumi jion katika michakato mizima ya kupambana na maisha magumu yaliyo sababishwa na serikali iliopo madarakani,,nika ahairisha shughuli zangu za kiuchumi'na nikahudhuria katika mkutano wa hadhara wa MH. JOHN MNYIKA katika maeneo ya Kimara mwisho jana,akiwa akiulizwa masaala mbalimbali ya maendeleo.

Ki ukweli maswali yalikua mengi moja ya maswali yaliyokuwa nguli, nayaita ni nguli kwa sababu mbunge wa CCM alieshndwa katika uchaguzi ulopita,alishndwa kuyatatua matatizo hayo NGULI, namnukuu MH, MNYIKA"nilipokua nikiomba kura mwaka2010 wazee wa kimara wakanambia kijana wetu tunakupenda sana ila ondoa agenda ya maji kwan utashndwa timiza.

Nikawajibu wazee wangu msiwe na wasiwasi sitashndwa nipeni kura zenu niwape raha"mwisho wa kunukuu,,hiyo ilikua n agenda yake alipokua akiomba kura na sasa amesha anza kulifanyia kazi suala hilo na ame ahidi pindi atokapo bungeni lazima azindue mradi wa maji, kulingana na mchakato n wapi alipofikia katika mchakato mzima wa wananchi kupata maji.

Amesema katika mji wa KING'ONGO Kimara na miji mingine iliopo kimara ambapo tatizo la maji limekua sugu kwa muda mrefu sasa litakwisha,na pia serikali inadai kwamba inampango wa kutengeneza barabara ya line nne hadi chalinze kuepuka msongamano wa magari,Mnyika amekanusha hilo kwa kusema"hakuna pesa katika bajet2010-15 inayo onyesha kuna pesa kwa ajili hiyo"bali kuna bajet ya pesa yakujenga barabara ya magari yaendayo kasi.

Naridhika nionapo kiongoz kama Mnyika anapopanda jukwaan na kuwa eleza wananchi waliompigia kura kwamba toka mlipo nichagua nimefanya hikiki na hiki na nimefikia hapa,sio kama v ongoz wengine wanaosubiri kipindi cha kampen mfano huu unafaa kuigwa na viongozi wengine.

TUONDOE KASUMBA ETI TUKICHAGUA CHAMA PINZANI HATUPATI MAENDELEO na pia yapo mengi aliyoyaongelea ila hayo nimachache tu kwa kuwa ndio yalikuwa matatizo ya muda mrefu.
 
Myika ni Jembe. Ubungo hawtaki tena CCM. Ubungo ilimpoteza mbunge Brayson, haijawahi kupata mbunge kama John.
 
Mnyika ni power tiller Huku kwetu tuna mbunge anitwa Jerome banahusi alikuwa meya wa temeke kipindi kilichopita hajawahi hata kujikuna akiwa huko bungeni tungempata mnyika angekiwa mbunge wa maisha
 
Mnyika anatia matumaini sana huyu jamaa. Nadhani wananchi wanataka kusikia ni nini mipango ya mbunge wao si kukaa nayo ofsini kwako hata kama ni mizuri kama hujawashirikisha haitakusaidia. Tunataka wabunge wa chadema hasa wa dar waonyeshe mfano maana itakuwa ndiyo ticket pekee ya kuyachukua majimbo mengine yaliyobaki 2015.
 
Mh. Mnyika tunakukubali, endeleza mapambano
 
huyu mtoto sound nyingi vitendo hakuna, anachofanya sasa kutengeneza shavu.
 
Mkigoma acha mawivu, wabunge 10 wa CCM ni sawa na John Mnyika mmoja, acha kumkatisha tamaa kijana acha na koma kabisa.
 
Back
Top Bottom