Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Akitoa maoni kuhusu mchakato wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Nchini unaoendelea Dar es Salaa, Msanii wa Bongo Fleva, Joh Makini amesema:
Ni haki ya Msingi ya Mwananchi aliyetimiza vigezo, kama hutajiandikisha utakuwa unawapa nafasi wengine wakufanyie maamuzi, wewe unatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, shiriki, Uandikishaji sio suala la kupata Kitambulisho pekee bali kushiriki katika kufanya maamuzi ya Kikatiba na Kidemokrasia.
Soma, Pia
Yule kichaa waliemuokota akichunga mbuzi huko porini ndio alinajisi demokrasia hapa nchini na waliorithi wanakenua na kuendeleza huo uhuni TU!Tatizo linalofanya watu wengine wamekuwa wazito kujiandikisha ni kwa sabu ya ukweli usiofichika kuwa kwa sasa hivi hapa Tanzania kura haina maana wala thamani tena, kwa utaratibu uliobuniwa na CCM mwaka 2019 na 2020 ambao ndiyo unatumika hadi sasa kama tulivyoshudia November 2024 wa kuengua wapinzani na kuiba kura na mshindi halali kutotangazwa kuwa ameshinda. Ni kupoteza muda kwenda kushiriki zoezi la kupiga kura wakati unajua kuwa Tume inakuja na matokeo yake mfukoni.Mimi kadi ninayo lakini kamwe sitakaa nipoteze muda wangu kupiga kura. Hata wanaojiandiksha wengi wanataka kupata tu hicho kitambulisho.Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kupoteza muda wake kupanga foleni tena juani au kwenye mvua kupiga kura. Ni CCM na serikali yake ndiyo imeondoa maana halisi ya kupiga kura. Inatumika karibu nusu Trilioni kwa ajili igizo la kupiga kura, ni bora tu hiyo hela ingeelekezwa kwenye huduma nyingine za maendeleo kuliko kuzitia kiberiti kwa uhuni unaoitwa uchaguzi.NO REFORM NO ELECTION.
Katika jambo ambalo namlaani Mkapa ni hili la kutuachia yule mwendawazimu, Mapdri na Maaskofu wa Kikatoliki walimuonya kuwa huyo ni kichaa akamkingia kifua.Yule kichaa waliemuokota akichunga mbuzi huko porini ndio alinajisi demokrasia hapa nchini na waliorithi wanakenua na kuendeleza huo uhuni TU!