Joachim Low na Muhaho wa world cup mwaka 2018

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Timu ya taifa ya Ujerumani ali maarufu kama Nationaelf(national eleven) au unaweza waita Die Mannschaft yani (the team) ni moja ya vigogo soka la ulaya kwenye ngazi ya mataifa ikiwa imewahi kuchukua kombe la dunia(worldcup) mara nne(4) ikiwa imepita miaka saba(7) tangu wachukue kombe lao la mwisho mwaka 2014 na mabingwa kombe la mataifa ya Ulaya(European championship) mara tatu (3) mara ya mwisho ikiwa mwaka 1996.

Katika kombe la mataifa ya Ulaya la mwaka 2016 nchini Ufaransa walitolewa na wenyeji Ufaransa katika hatua ya nusu fainali kwa magoli mawili kwa bila yaliyofungwa na mchezaj aliyekua kwenye ubora sana Antoine Griezman. Hakukua na malalamish sana kwa kocha Joachim Loew maana walifungwa na timu ilokua kwenye ubora sana.

Changamoto kwa Loew zikaaanza Ilipotimia mwaka 2017 katika mashindano ya kombe la mabara (Confederations cup) ambapo aliwaach wachezaj wengi alokua nao kwenye kikosi kilichochukua kombe la dunia 2014 na kushiriki Euro 2016 huku akiita vijana wachanga kabisaa.

Wengi walibeza sana chaguz yake ya kikos huku mwenyewe akisema anawapumzisha na kuwaita wachezaj watatu(3) tu kati ya walioshinda kombe la dunia 2014 wakiwa ni mabeki Mathias Ginter na Shokordan Mustaf pamoja na nahodha wa kikos chao Julian Draxler.

Wachezaj kama Manuel Neur na Marco Reus waliachwa sababu ya majeraha huku nyota kama Toni Kroos, Mario Gotze(goli lake kwenye extra time liliwapa ubingwa 2014), Muller, Hummels, Ozil na Khedira wakipumzishwa.

Loew akatembea na damu changa ikiwahusisha werner, sebastian rudy, Sane, sandro wagner, leon goreztka, julian Brandt na wachezaj kama diego demme na emre can wakiwa kwenye kosi hilo la Die Mannschaft.Katika fainal wakakutana na Chile ambae walimpga gol moja bila likiwekwa kimian na Lars stindi dk ya 21 huku Chile wakitawala mchezo kwa dakika karibia zote za mchezo japo bahati haikua upande wao.

Loew alisifiwa sana kupata hilo kombe japo kwa mechi chache kwasababu alitumia damu changa sana ilihal hapo mwanzo alipigwa vita kwa chaguzi yake.

Ujeruman kwa mafanikio walopata kwenye kombe la mabara 2017 itegemewa kua itafanya vzur sana kwenye kombe la dunia 2018 na itafika mbali kwa maana itakua na kikos bora saaana kutokana na vipaji vipya vilivyoonekana kwenye kombe la mabara pamoja na wakongwe.

Loew katika teuz yake akamtema Leroy Sane aliyekua bora saaana katika kikos chake na kumuita kijana Julian Brandts ambaye hamna anayemdai maana alicheza vzur sana pamoja na Timo werner.

Ujeruman mech ya kwanza vs Mexico wakafa goli moja bila inayofuata wakashinda 2 vs 1 sweeden na ya tatu wakapigwa 2 vs 0 dhid ya South Korea na kumaliza wa mwisho kwenye kundi lao na kutolewa kwenye makundi kama France alivyotolewa kwenye makundi 2002, Italy akitolewa 2010 na Spain alivyotolewa mwaka 2014 huku wote wakiwa mabingwa watetezi.

Tatzo la Loew 2018 liligusa maeneo mawili makubwa ambayo ni mfumo na chaguz ya kikos ya kikos kinachoanza. kwa miaka takriban nane mfululizo alikua anapenda sana kutumia mfumo wa 4 2 3 1 na kutumia target man ambaye alikua ni Miroslov Klose na mbadala wake Mario Gomez.

Katika kombe la dunia 2018 mechi zote alianza na Werner ambae hana elements za utarget man na ambae anapenda sana kufanya mikimbio pemben sana kulko katikat katika kufungua mabeki na kupata space ya kucheza huku Mario Gomez aliyekua Frankfurt akisugua bench. Hii iliathir sana Ujeruman kwenye finishing maana pia Muller Hakua kwenye kiwango kizuri. Pia katika mech hyo ya kwanza Hummels alikaririka akisema timu imecheza vibaya sana hasa katikati walkua uchi sana akigusia kiungo cha Kroos na Khedira kitu kinachosemekana kocha hakupenda na kumuweka bench mech inayofuata na kuanza na Rudiger na Boateng.

Pia chaguz la kikos baada ya kupoteza mech ya kwanza, kwa kuanza na Rudy badala ya Khedira na Reuc badala ya Ozil kuliwapa sana nguvu Ujeruman na kupata matokeo vs Sweeden tena wakimaliza pungufu badala ya Boateng kula umeme.

Kilichoshangaza ni kwenye mech ya mwisho ambapo kocha alifanya mabadiliko matano kwenye kikosi kilichoshinda vs Sweeden huku akimrejesha ndani Khedira aliyekua flop, Ozil, Goretzka, Hector na Hummelz wakichukua nafasi za Muller, Rudy, Draxler, Boateng na Platternhard na kupelekea Die Mannschaft kufa goli bila bila. Kwa ufupi mwalimu alihaha

Marco Reus baada ya kuondolewa kwenye makundi alikaririwa akisema nilipumzishwa mech ya kwanza kwa ajili ya mechi zinazofuata kumbe mech ya kwanza ndo ilkua muhimu sana kwetu

Baada ya kombe la dunia 2018 Loew aliwapiga chin Hummels, Boateng na Muller kwenye kosi lake la taifa.

Loew n timu yake ya taifa katka kipind hiki cha karibun hawana rekodi nzur huku wakiwa na rekodi mbaya ya Kufungwa goli 6 bila vs Spain kwenye Uefa nations league na wenyewe ushindi wao mkubwa kwenye mech za karibun ukiwa 7 vs1 dhidi ya Latvia ambao ni vibonde.

Loew anakikosi bora sana kwa sasa on paper. Japo inaonekana eneo lake la ushambuliaj halipo vzur sana kistats katika mechi za karibuni. Huku gnabry, Sane, werner, Havertz, Volland, Draxler, Florian wakiitwa na kurud kwa Muller kukitegemewa kurudisha makali ya safu hii ya ushambuliaji.

Loew kwa sasa kaja na mfumo wa back 3 4 3 au 3 5 2 huku akiwatumia hasa Kimmich, Gundogan na kroos eneo la katikat au Kimmich eneo la wingback pamoja na Gosens ikiwa ni kutafta balance katika kukaba na kushambulia huku akitegemea nguvu ya Sane..gnabry,,Havertz na Werner kwnye kushambulia akiweka mbali mategemeo ya target man, anataman sana kuipa nchi yake fahari nyingine huku akiwa ametangaza kustafu mara baada ya michuano hii.

Yupo kundi gumu sana lenye timu kama Ureno na Ufaransa. Safar yake ya kusafisha nyota inaanza kesho vs Ufaransa ambao ni wamoto saaana.

Namtakia kila la kheri katika mechi yake hyo ya kwanza.

#Adios Amigos
 
Mimi
Kesho namdhalilisha Low hataamini macho yake kama sio 7-0 basi 5-0 zitamtosha...I'm sorry Toni Kroos.
 
Back
Top Bottom