JNIA: Wanne wafukuzwa kazi kwa wizi wa Mafuta ya Ndege na Mizigo ya wateja

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Serikali imewasimamisha kazi maafisa watatu wa Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya ndege na mmoja kati yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni ya Swissport.

Akizungumza katika ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika Viwanja vya Ndege vya Mwalimu J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni amewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Khalfani Kisana na Mussa Mandauli ambao walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya ndege wakiwa na gari la Serikali lenye usajili namba STJ 2948.

Askari mwingine aliyejulikana kwa jina la Abbas Mwanza alisimamishwa kazi kwa tuhuma za kosa la kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport, Lucas Maganda kwa kosa la kuiba mzigo wa abiria.

Akiwa katika kiwanja hicho Mhe.Masauni amekagua utendaji kazi katika idara ya Uhamiaji, Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza viongozi wa idara hizo zilizopo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Source: Maafisa wasimamishwa kazi kwa kushiriki kuiba mafuta ya ndege na mizigo ya wateja JNIA - wavuti
 
wanaiba mafuta ya taa wataacha mabeg ya abiria kweli huyo achunguzwe zaidi kwa upotevu wa mabegi hapo.
 
Wanauza rejareja kwa wamiliki wa ndege ndogo na helikopta.
Imenimbisha kuna kesi moja ya wafanyakazi wa Atcl walikamatwa asubuhi wanakinga mafuta kutoka Kwenye tanki la ndege kabla ya ndege kuanza kufanya kazi hii ni aibu kubwa.
 
Wana ndege nyingi sana pale za kukodi ndio wateja wao wakubwa! Ni aibu sana jamani na inaonekana ni kamchezo ka siku nyingi hadi wamezoea na kupakia kwenye gari la serikali! Ni ka mtandao......wamechoka kuvumiliana uhalifu safi sana
 
Ni aibu sana kwa wafanyakazi wa Swissport kupasua mabegi ya watu,kuiba vitu na kuchukua rushwa pamoja na customs
 
Back
Top Bottom