JNHPP kuifanya Tanzania kinara katika kuzalisha umeme Afrika Mashariki

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
JNHPP KUIFANYA TANZANIA KINARA KATIKA KUZALISHA UMEME AFRIKA MASHARIKI

Umeme wa maji (Hydropower) ndio chanzo namba mbili cha nishati ya umeme katika nchi za Marekani na China. Maendeleo Duni Afrika yanachagizwa na ukosefu wa nishati ya umeme, takwimu zinaonyesha kuwa nchi zote za Afrika kwa pamoja zinauwezo wa kuzalisha karibu asilimia 20 pekee ya umeme unaozalishwa na Nchi moja ya Marekani.

China inategemea umeme katika mabwawa zaidi ya 15 yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya Megawati 2000 kila moja, huku Bwawa lililoko katika mto Yangtze pekee likizalisha Megawati 22500. Hivi sasa China imewekeza mabilioni ya fedha katika kujenga Mabwawa takribani 10 ili kuendelea kunufaika na umeme salama na wa gharama nafuu.

Tanzania iko katika hatua muhimu za kukamilisha ujenzi wa Bwawa (JNHPP) litakaloweza kuzalisha Megawati 2115, kukamilika kwa JNHPP kutaifanya Tanzania kuwa kinara katika kuzalisha umeme mwingi zaidi Afrika Mashariki.

Ongezeko la uzalishaji umeme wa gharama nafuu ni kichocheo muhimu kwa Viwanda na wawekezaji wengi huvutiwa na factors kama hizi katika kutafuta maeneo mapya ya uwekezaji. Hongereni sana Watanzania kwa hatua hii katika kukuza uwezo wa nchi yenu kuzalisha nishati ya umeme.

Mradi huu uliopo katika mto Rufiji ulianza rasmi kutekelezwa mwezi June mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi June mwaka 2022.
 
Back
Top Bottom