JK uko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK uko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Dec 27, 2011.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  JK aliingia madarakani kwa mbwembwe sana na ahadi lukuki na akiwa amebeba matumaini makubwa ya WaTZ. Tatizo yote ameyatelekeza na kuwaacha wananchi wakiwa hawana kimbilio wala pa kusemea. WaTZ kuandamana sio asili yetu ila unapoona tunaweza kuandamana, machinga wanapigana na mgambo na polisi, kule Mbeya juzi tu watu wanarushiwa mabomu ya machozi na wao wanayadaka na kuwarushia polisi,JUA KUWA TUMEPOTEZA TUMAINI NA NCHI YETU NA UTAWALA WAKE.
  -Nchi inayolima miwa kibao inakuwa na uhaba wa sukari, tunanunua kilo kwa shs 3000 kama enzi zile za NMC kununua kwa mstari tena unaambiwa usinunue zaidi ya kilo 2.,
  -watu wanagoma kuuza mafuta wananchi wanateseka nchi nzima na serikali imekaa kimya tu,
  -watu wanaiba hela za serikali (EPA) na wanashauriwa warudishe then wanaendelea kufaidi maisha na serikali ipo tu
  -Madini yanabebwa bure na wananchi wanaachiwa maji yenye madhara kwa afya zao na serikali inatabasam tu
  -Watu wanaingia mikataba ya hovyo kama richmond na gharama zake anabebeshwa mwananchi
  -Maisha ya mTZ yanazidi kushuka thamani kila siku
  -Hospitali mtu anaenda kujifungua anaambiwa aende na pamba na gloves
  -shule za msingi madawati hamna, walimu hamna, vitabu na vitendea kazi vingine hamna
  -Vyuoni mikopo wanapewa watoto wa wakubwa na makabwela wananyimwa, migomo kila siku na ukigoma unafukuzwa
  -Wahitimu kibao mtaani ajira hamna
  -Serikali inanunua ma V8 ya 200mil. lakini bado inaongoza kuomba misaada nje na mikopo kila siku
  -Walimu wanaidai serikali malimbikizo miaka nenda rudi lakini yenyewe inaandaa sherehe za uhuru wa miaka 50 wa nchi ambayo haipo (Tanganyika) kwa kila wizara- wengine wanahama toka dar kwenda kufanyia butiama
  -Mishahara midogo kwa watumishi wa serikali na binafsi
  -Uwekezaji ambao unawanufaisha wageni tu, waTZ wananyanyaswa kwenye migodi na makampuni ya wageni ya ujenzi lakini hawana pa kusemea maana serikali na vyama vya kuwatetea vimeshatiwa mfukoni na wawekezaji
  -SERIKALI HATA KUWASAIDIA WALIOPATWA NA MAFURIKO DAR IMESHINDWA, CHA AJABU HATA MISAADA INAYOTOLEWA NA WASAMARIA WEMA WANASHINDWA KUILINDA NA INAIBIWA


  Nauliza JK yuko wapi?
   
 2. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani useme unataka kitu gani?

  Kwani haujui kuwa JK yuko Ikulu na kwa sasa anapumzika Mbugani amechoka kufanya shughuli za kuwaletea Watanzania Maendeleo? Sema staright forward kipi kifanyike kwani ukishajua alipo ndo hayo matatizo uliyoyalist japo kwa uchache yataisha?

  Kwa mfano, hapo ulipo umeanza hata harakati za kuhakikisha CCM hairejei madarakani kwa kuanza tu kuwashawishi vijana, wazee na marafiki zako kwa hoja za msingi au unasubiri hadi tarehe za kampeni zitangazwe? Je, una kadi ya CDM (manake vingine ni vipandikizi vya CCM)?

  Nadhani hatuhitaji kujua JK alipo, tunahitaji kuanza kupambana na CCM kuanzia sasa, muda umeisha na Watanzania tumezubaa muda mrefu watu wanakufa kwa umaskini unaosababishwa na viongozi wetu ambao vichwa vyao vimejaa MAJI badala ya Ubongo. Viongozi wanaofikiria "mimi" badala ya "sisi".

  Nawasilisha.
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yuko magogoni
   
 4. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Magogoni hayupo maana alishamuuzia George Bush. Pale wanakaa walinzi wa mji mpya wa Kigamboni
   
 5. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Aisee kadi ya CDM sina maana hawataki kufungua matawi huku Mtwara vijijini. Na kujiunga online bado ni kitendawili. Waambie wasambaze timu ije kusini mwa Tanzania maana CCM imechokwa na CUF wanajaribu ila kwa kuwa walishafunga ndoa na CCM ndo hivyo tena. Kuna wanachama tusio na kadi za vyama wengi huku, waje tu
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ni dhambi kubwa sana kutumia matatizo ya wananchi kama daraja kufanya ushawishi wa kisiasa.kikwete yupo anashirikiana na watendaji wake kuwahudumia watanzania wote ukiwamo wewe unaeandika uzushi hapa.sukari ni tatizo ktk nchi za afrika mash.kenya inauzwa ef4400
  uganda 5000.serikali inashirikiana na wadau kuwasaidia waathirika wa mafuriko nyie majina kapuni mnaenda kuiba ili ionekane govt imeshindwa kusimamia.tunazo tarifa zenu.acheni uchochezi.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  yani umeandika unafiki utafikiri ni mzalendo na una uchungu na tanzania, siasa bwana.
   
 8. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  .
  Wewe gamba lako limeunganika na ngozi. ndio nyie mkipewa ubwabwa na kanga mnauza kura zenu.
  Pole sana
   
 9. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hojatete, kwenye hii forum huwa tunajibu hoja kwa hoja. Katika pointi yangu ipi ambayo ni ya uchochezi au ya kisiasa??
  Jibu moja baada ya nyingine ili nione wapi serikali imejitahidi na mimi naleta uchochezi.
  Mh nilisahau, serikali imejitahidi kuuza twiga wetu nje ili watalii waishie Qatar badala ya kuja Tanzania
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Yuko Msoga kwenye mdundiko.
   
 11. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  JK yupo magogoni anakula bata na kujifariji kwamba hakuna hatari yoyote itamfika!
  Ole wake!
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwacheni Karudi Mapumzikoni Serengeti kaangalia Mafuriko imetosha
   
 13. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Bitabo,
  Mada, hoja yako haijakamilika, ulitakiwa uanze na Utangulizi, Body na Conclusion, vingine Mada, hoja zako hata ziwe na mshiko gani zitakuwa zinaelea tu juu na hata wachangiaji tutashindwa kukuelewa Ujumbe wako
  hapa wachangiaji tukisoma tunaona umeshambulia tu, ujasema nini kifanyike, nini kisifanyike, maoni yako juu ya mstakabadhi wa Nchi na mengineyo kama ushauri wako n.k
  Nawakilisha   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  shida siyo kujua jk aliko;swala hapa ni kwa nini tusiende kumtoa huko aliko
   
Loading...