JK, Pinda amechoka, mwache apumzike!

JK, Pinda amechoka, mwache apumzike!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,266
RAIS wangu, wahenga walisema: "Kinywa kiliponza kichwa!" Hivi ndivyo inavyotokea sasa katika nchi yetu. Waziri Mkuu wetu, Mizengo Pinda, ametoa kauli nyonyegefu inayoififisha serikali na kuifanya ionekane kama zimwi mla watu mbele ya wananchi wake.

Amesema: "Tumechoka". Kwa sentensi iliyonyooka ni kwamba waziri mkuu amekiri hadharani kuwa serikali imechoka!
Baba kwa kuwa waziri mkuu amethibitisha pasipokuacha shaka kuwa mmechoka; pumzikeni! Dereva akichoka hupumzika.

Aking'ang'ania kuendesha anatafuta kuua watu.

Mtajikuta mnaua watu! Mtajikuta na nyinyi mnaanza kung'oa watu meno na kucha bila ganzi! Si mmechoka! Baba pumzikeni! Maovu haya hayatawasaidia chochote zaidi ya kuwatengenezea visasi vitakavyofanya mwisho wa maisha kuwa wa kuhuzunisha na majuto ambayo hayatawasaidia kitu!

Akisisitiza jinsi mlivyochoka waziri mkuu akaongeza: "Hatuna namna nyingine ya kufanya". Yaani mko hoi bin taabani! Kwisha kabisa! Ukishaishiwa mpaka ukakosa namna nyingine ya kufanya unakuwa sawa na mfa maji.

Unatapatapa tu! Unakumbatia hata mzizi ambao na wenyewe umezama kama wewe. Haikubaliki nchi iendeshwe na wanaotapatapa! Ni jambo lililo wazi, ukishakosa namna nyingine yoyote ya kufanya maana yake huwezi tena kuongoza, hufai. Pumzikeni msije mkaua watu!

Rais wangu, mchoko wa akili wa wenye mamlaka ni maafa na maangamizi kwa waliochokwa. Anathibitisha kuwa wamefika mwisho wa fikra! Hawawezi kufikiri tena zaidi ya hapo. Wamechoka. Hawana namna nyingine ya kufanya.

Kilichobaki wananchi, ‘wapigwe tu'! Utaishia kuua watu ukidhani watatishika kumbe ndiyo unajimaliza mwenyewe! Sasa moshi wa mabomu ya machozi umekuwa sawa na moshi utokao dampo. Milio ya risasi na milio ya honi ya wanaotaka kupishwa haitofautiani katika masikio ya waandamanaji.

Ole wao waliowafanya wananchi wazizoee silaha! Ni mjinga peke ndiye hajui kuwa baada ya hapo wahanga watakuwa kina nani. Pinda kama ni kweli umechoka pumzika ndugu yangu! Uking'ang'ania zaidi ya hapa maafa utakayosababisha hayatakupitia kando!
Hakuna jehanamu yenye mateso makali hapa duniani kama kiongozi kuchukiwa na wananchi anaowaongoza! Ndugu Rais jiepushe baba na wapofu wanaodhani wanaweza kumuua nyoka kwa kumchapa na fimbo kwenye makalio yake!

Mtu unajisikiaje kuwa waziri mkuu wa kwanza tangu nchi hii ipate uhuru kushitakiwa kwa uhalifu mahakamani na watu wako mwenyewe?

Muda wako mwingi sasa itabidi uutumie kujinasua katika kesi inayokukabili mahakamani badala ya kuwatumikia wananchi.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, "Pinda aburutwa mahakamani."

Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu ya Oxford, toleo la pili neno buruta au burura maana yake ni, ‘vuta kitu kilichokuwa chini kikigusana na ardhi; gugurusha au kokota'.

Hivi ndivyo inavyoburutwa mifugo kama mbuzi inayokataa kwenda inakopelekwa! Ni waandishi wetu ndio wamemweka Pinda katika kundi la vinavyoweza kuburutwa au amejiweka mwenyewe?

Kama umeudhi watu wako kiasi cha kuwafanya wakutoe katika watu, wakuweke katika vitu, kung'ang'ania kuwatawala ni kuitafuta zahama! Kinachofuatia hapo, ni kufukuzwa kwa aibu kama anavyofukuzwa Mswahili mwingine yeyote asiye na anwani. Vyeo hivi ni dhamana, siyo vyetu! Tunawajibu wakulinda heshima ya vyeo hivi!

Rais wangu, waziri mkuu ni jirani yangu kwa maeneo tulikotoka. Kwa miaka tuliyonayo sasa ukuaji wetu kule vijijini ulifanana. Mwenzangu baba yake alikuwa mkulima.

Mwenzake baba yangu alikuwa mfanyakazi wa hospitali akichoma watu sindano na kuwafunga vidonda.

Sekondari tumesoma shule ileile. Maadili tuliyolelewa ni yaleyale.

Maisha ya anasa tuliyonayo sasa ya kula bure, kuvaa bure na hata kuwa na uwezo wa kuagiza maangamizi juu ya wengine, yasitupumbaze tukasahau tulikotoka na hasa maisha tuliyokulia!

Mwenzake kabla ya kuanza shule nilichunga ng'ombe na kisha nikachunga mbuzi. Mbuzi humkomaza mchungaji wao. Bado muda mfupi sana tutakuwa huko tena tulikotokea wakati huo sasa nguvu za mwilini zikiwa zinatuishia.

Wapambe wetu tunaongozana nao sasa tutakuwa hatuko nao tena! Badala yake wale wote tuliowadhuru kwa maagizo yetu watatoka huko waliko kila usiku na kuja kuungana nasi katika ndoto zetu! Usingizi wetu wa kila siku utakuwa wa mang'amung'amu! Tusipobadilika sasa, tutayamaliza maisha yetu katika dhiki kuu!

Abarikiwe mzee Madiba, Baba Nelson Mandela, ambaye hadi leo bado analala katika kitanda chake cha mauti akiwa amejawa na amani kubwa kifuani mwake na furaha ya kweli katika moyo wake huku kichwani mwake akiwa na matumaini ya kumwona Muumba wake baada ya muda mfupi ujao!

Anajihisi yuko sehemu ya mapokezi yake Mwenyezi Mungu akisubiri kumwona Muumba wake baada tu ya malaika wake watakapomwondelea uzio! Haiwazii hukumu ya Mungu bali anaufurahia mwanga wa milele utakaomwangazia!

Hapa duniani sisi wote ni wapitaji tu! Makao yetu ya kweli yako kule aliko Baba! Ndugu waziri mkuu kumbuka, u mavumbi na mavumbini utarudi! Ukiona umefika kumbuka ulikotoka kabla ya kutoa thamani ya utu wa watu wengine!

Haya yote ni ya dunia, yanapita!

Rais wangu ‘Liwalo na liwe' ni kauli isiyoweza kusahaulika na yeyote anaye mcha Mwenyezi Mungu. Makali ya kauli hii yalishinda makali ya ncha ya upanga!

Kila aikumbukayo kauli hii, hukumbuka unyama ulioifuatia.

Moyo wake hupasuka kama uliochomwa na kitu chenye ncha kali mithili ya mkuki uchomavyo moyo wa adui! Liwalo na liwe ilifuatiwa na kitendo cha kinyama ambacho Watanzania walikuwa hawajawahi kushuhudia! Unyama ule hauwezi kuelezewa na mtu yeyote kwa ufasaha kabisa katika lugha yoyote! Kitendo kiovu kilichodhihirisha nguvu kubwa aliyonayo shetani.

Ndugu Rais, wako watu wanaamini kuwa Mungu wa siku hizi humuadhibu mwanadamu hapahapa duniani. Ukiwa na imani potofu unaweza ukadhani shetani anamsaidia Mungu kutimiza malengo hayo.

Serikali ilikataa kuhusika na unyama ule. Wananchi wakasema basi! Kukanusha hakuna uhusiano wowote na ukweli kuwa ulihusika au hukuhusika, lakini wananchi wangesahau!

Sasa Rais wangu, kama siyo nguvu ya shetani huyu aliyeenda kumkurupua chizi wa watu kule kanisani alikokwenda kusali, alitumwa na nani? Kumfungulia kesi mahakamani kuna maana moja tu; kuwakumbusha wananchi na taifa kwa jumla unyama wa kauli ya liwalo na liwe kila kesi itakapotajwa! Hasira za wananchi zitaishaje? Shetani ana nguvu kubwa japokuwa hamfikii Mwenyezi Mungu.

Wapinzani sasa wanaongea juu ya mabadiliko ya uongozi 2015. Cha kushangaza kila unayemuuliza wamejipanga vipi, hana jibu. Kama hivi ndivyo sielewi ni kwa vipi wanashangaa kusikia Robert Mugabe ameshinda uchaguzi Zimbabwe.

Ni kipi kingemfanya asishinde? Mazingira ya uchaguzi wa Zimbabwe ndiyo hayohayo yaliyopo hapa nyumbani. Ni kipi kitamfanya Mugabe wa Tanzania asishinde 2015? Wanadhani ushindi unapatikana kwa kufuata midundo na mihemko ya mioyo yao.

Upinzani wa hapa kwetu ungeleta maana kama ungekuwa kitu kimoja. Kwa hakika 2015 wangepeta kwa kishindo. Tukiendelea na hali hii hii iliyopo hadi 2015 ushindi kwa upinzani utakuwa kama mvua ya kiangazi. Hutokea kunyesha lakini si kitu cha kawaida.

Ushindi wa uchaguzi wa madiwani mkoani Arusha ulipaswa kuwapa funzo wapinzani kuwa Mugabe wa Tanzania (chama tawala) bado ngangari.

Alitibuliwa na vijana wake wawili ambao kwa upeo wao finyu wanadhani kampeni ni uhodari wa kutukana matusi hadharani.

Nasema hadharani kuwa kama viongozi wenye busara kubwa, Makamu Mwenyekiti Bara, Phillip Mangula, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, wazee Salim Ahmed Salim, Prof. Sarungi na wengine hawatamlazimisha mwenyekiti wao kuwaondoa vijana wake wawili, mabingwa wa matusi kwenye safu ya uongozi, chama kimeuawa!

Matatizo yote ya chama yanaanzia ndani ya ofisi ya mwenyekiti. Ushalubalo na ufuska umeua vyama vingi sana hapa duniani! Hawa ndio wanaowatia nguvu kubwa wapinzani.

Rais wangu chama kikiwa katika hali hiyo na huku serikalini kauli ndiyo hizi kutegemea kuendelea kuongoza, si sawa na kutegemea nguvu za giza?

Pinda asiogope machungu ya kujiuzulu. Kwanza ana mfano hai mezani pake wa mtangulizi wake. Waziri Mkuu Edward Lowassa alijiuzulu. Ilimlazimu kufikiri sana kupata sababu ya kuwaeleza Watanzania kwanini aliamua kujiuzulu kwa sababu ndani ya kifua chake hakuona aliloikosea nchi yake au watu wake!

Alisema tu sababu ilikuwa ni uwaziri mkuu wake! Nakiri wengi hatukumwelewa wakati ule!

Wahenga walisema: "Muda huponya". Leo hii, baada ya mambo yote kuwekwa hadharani wenye moyo safi wanakiri kuwa Edward alikuwa jembe! Tangu alipokubaliwa kujiuzulu nchi ilienda kuzimu na imebaki huko hadi leo!

Tulibaki kufanyishwa utoto mwingi, ubishoo na ushalubalo! Mafisadi wake, kwa aibu kubwa wameinamisha nyuso zao chini nao wanazeeka kwa haraka!

Mwanamwema Sima wa Dar es Salaam aliniandikia ujumbe ufuatao: "Habari. Tarehe 9-12-2009, katikati ya kelele za Mwakyembe, Samuel Sita na kundi lao nilikuwa nyumbani kwako. Tukiwa chini ya Mwembe ukaniambia, hawa watu si wapambanaji dhidi ya ufisadi bali ni waovu wanaotumia uelewa wetu mdogo kutuibia kwa kutuonyesha wenzi wenzao! Sasa naamini na nakumbuka kila ulilonitamkia. Ubarikiwe sana."

Kwa kuliona hili Mwenyekiti wa kundi machachari la G 55 mwaka 1993 mzee wetu, Mateo Qaresi, amesema Tanzania kama taifa halina dira wala mwelekeo na matokeo yake mambo yake yamekuwa yakienda bila utaratibu.

Akitilia shaka uelewa wa viongozi wetu aliuliza: "Hivi hawa viongozi wanajua tunakoelekea? Leo hii ukiulizwa dira yetu nini hakuna anayejua, bali tunajiendea tu!" Ili kuliokoa taifa na tawala za aina hii ameshauri kinga ya rais ya kutoshitakiwa iondolewe akidai kuwa marais wa sasa wamekuwa na viburi na hawashauriki.

Mizengo Pinda hatapata shida ya kuwaeleza Watanzania sababu ya kuachia ngazi. Kufikishwa mahakamani peke yake na watu wako, kwa mtu mwenye nafsi iliyo nyofu inatosha kuondoka!

Hawa ni wananchi wako mwenyewe ambao wanakuonyesha wazi kuwa hawautaki utawala wako, unawalazimishaje?

Kauli ovu zinakimaliza chama! Kuchoka si kosa, ni hali mojawapo katika maisha ya mwanadamu. Busara, ukichoka pumzika!

Rais wangu, kwa dhamira aliyoionyesha waziri mkuu dhidi ya wananchi, Watanzania sasa wanaanza kuwakumbuka mawaziri wakuu waliomtangulia, mmoja baada ya mwingine.

Katika wote hawa hakuna hata mmoja aliyewaachia Watanzania kumbukumbu ya kujutia kama inavyotaka kutokea sasa!

Hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa tishio kwa maisha ya watu wa nchi hii aliowaongoza!

Hakuna anayekumbukwa kwa uovu! Iweje mpaka mawaziri wakuu wengine waisikitikie kauli hii ovu iliyotolewa na waziri mkuu wa sasa! Wote waliondoka salama na sasa wanaishi kwa heshima kubwa katika jamii yetu!

Kina Edward mpaka leo bado wanakumbukwa kwa utendaji kazi wao mahiri! Mizengo Pinda atakumbukwa kwa hili! Baba Pinda, usiinue pembe zako juu wala usinyoshe shingo yako kwa kiburi kwa maana imeandikwa kuwa Mungu wako hayuko mashariki wala magharibi!

Rais wangu, wakale walisema kuwa, kwa asiye na busara akipewa mamlaka makubwa humlevya, naye hutumia mamlaka hayo kujitengenezea mwenyewe mwisho mchungu, akamalizie siku zake za mwisho za maisha yake katika upweke wa kutisha huku akiwa amegubikwa na huzuni kuu yeye na familia yake!

Ukiwa unalia hadharani, bado wengine wanajiandikisha kusema hawana imani na waziri mkuu, huku wengine wanakuburuta mahakamani, jua umekuwa kero kwa watu wa Mungu! Mwenyezi Mungu hapendi!

Usingoje aibu pale Muumba wao atakapokujibu kwa hasira kwa niaba yao! Kuachia ngazi ni kulinda heshima yako mwenyewe lakini muhimu, kulinda heshima ya nchi na taifa kwa ujumla!

Source: Paschally Mayega: Tanzania Daima 07/08/2013
 
Tanzania ni nchi pekee mtu anang'ang'ania cheo kilicho mshinda, shame on us.
 
ngoja watoto wake waje hapa...kina hammy dada utaifa badae . ritz and other
 
Ndugu Mayega nakuheshimu sana ila naomba uelewe kwa sasa serikali yetu ipo kwenye msimu wa kupiga,na unachofanya wewe ni kupingana na sera tukufu za chama tawala zukisimamiwa na serikali sikivu ya CCM/Magamba Club.

Sasa na mimi nimeshawaagiza Comrade Chagonja,Kamuhanda na Film Producer of police(Mr.Kova) kwamba mpigwe tu kwani tumechoka.

Ndugu wanaJf msimu wa kupiga kwa sasa tumeanzia ukanda wa pwani,na sasa tupo Mtwara. Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Tarime na Mwanza bado police tumekaa kama kamati na tunapanga kutumia strategy inaitwa General attachment.
 
Unalalamika au unafanyaje?
 
gazeti la udaku na habari za kuokota na kuzua mambo.
 
Afadhali anayengang'ania kuwepo, kuliko anayetaka kuwepo wakati hana uwezo.

You write like a headless chicken, do you use your sitting facilty for thinking? anayetaka kuwepo hana uwezo kwa kipimo kipi sahihi, maana aliyepo ndo kapimwa kwa majukumu alopewa na ameshindwa, sasa anayetaka kuwepo hana uwezo kwa kufikiria tu au? poor thinkers do live today because it is declared illegal to exterminate them.
 
Ndugu Mayega nakuheshimu sana ila naomba uelewe kwa sasa serikali yetu ipo kwenye msimu wa kupiga,na unachofanya wewe ni kupingana na sera tukufu za chama tawala zukisimamiwa na serikali sikivu ya CCM/Magamba Club.

Sasa na mimi nimeshawaagiza Comrade Chagonja,Kamuhanda na Film Producer of police(Mr.Kova) kwamba mpigwe tu kwani tumechoka.

Ndugu wanaJf msimu wa kupiga kwa sasa tumeanzia ukanda wa pwani,na sasa tupo Mtwara. Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Tarime na Mwanza bado police tumekaa kama kamati na tunapanga kutumia strategy inaitwa General attachment.
Kweli kabisa kamanda tena nauwakika makao makuu ya hiyo kambi yapo Arusha. Alafu nasikia walikua mapumziko kupisha mwezi mtukufu, hivyo kwanzia jumamosi wanarudi kazini kazi ni moja tu "KUPIGIA TU"
 
JAMAA alimteua MUTOTO YA MUKULIMAAA akijua vyema tu kuwa kachoka lakini kwake huyu babu WM na babu aliyesoma nuclear physics ni bora kuliko wajanja aina ya KARAMAGIIIII NA EL RICHMOND!
 
Wapiga kura wataamua cha kufanya ifikapo 2015 maana anaowalamikia wameziba masikio na pamba machoni wamevaa "miwani ya mbao" hawataki kuona kinachoendelea kwa Watanzania.
Wamesema wamechoka tumesikia kwa maskio yetu,tutawaonyesha njia ifikapo 2015 wakapumzike.tunawatakia mapumziko mema!
 
Ukiua kwa upanga,utauwawa kwa upanga! fikra potofu kama za pinda ni muhimu kwa sasa ktk nchi kwa kuwa zinaharakisha mabadiliko! mwalimu,pole sana!lakin muda umewadia mungu anawatumia viongozi dhidi yao! Nchi yangu kwanza!
 
Back
Top Bottom