Jk na mazingaombwe ya fedha za epa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk na mazingaombwe ya fedha za epa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamakabuzi, Sep 26, 2008.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwanza, kuna kauli ya waziri wa fedha Mustafa Mkullo kwamba fedha za EPA si za serikali. Kauli hii haijapingwa na JK

  Pili kuna suala la fedha hizo ni kiasi gani? Wengi tunajua kuwa fedha zilizoibwa mwanzoni ni bn 133 na baadae zikaongezeka bn 5. Lakini kuna kauli ya JK kuwa mfuko huo ulikuwa na fedha bn 600, ni kiasi gani halisi kipo hivi sasa – hatujui.

  Waziri wa fedha alishasema fedha zitakazorudi hazitazidi bn 100 na JK hajakanusha hilo.
  JK anasema fedha za EPA sasa zitapelekwa kwenye kilimo. Nasisitiza ni fedha za EPA na siyo siyo zile tu zitakazorudishwa ndizo zitaenda kwenye kilimo, maana yake fedha zote za EPA zitapelekwa kwenye Kilimo – maana yake bn 600.
  Waziri wa fedha alisema hizi fedha ni za makampuni binafsi, JK ameliunga mkono hilo na kusema hatarajii kampuni yoyote kuja kudai fedha hizi! Akaongeza, kama kampuni yoyote itajitokeza basi serikali itailipa!

  Haya sasa ndiyo mazingaombwe:

  Nani ameipa mamlaka serikali kugawa fedha zisizo zake? Je tunarudi kwenye utaifishaji? Hapa jibu ni hapana - serikali haina mamlaka ya kugawa fedha zisizo zake.

  Ni kampuni gani halali inayoweza kuacha kuidai serikali fedha zake? Labda ni kampuni ambayo hizo fedha haikuzipata kihalali na hivyo kuogopa kudai. Au labda kama kampuni itakubaliana na serikali kusamehe deni hilo. Hapa JK alipaswa kutupa takwimu kuwa mazungumzo na kampuni hizo yanaendelea juu ya kusamehe deni hilo; lakini kusema tu kuwa hatarajii kama makampuni yatakuja kudai, ni ndoto za alinacha. Na hata msamaha unapotolewa huwa anayesamehe anaelekeza msamaha huo ufanye nini - maana yake lazima fedha hizo zipatikane na zielekezwe huko.

  Kama kampuni zote zilizochanga fedha zitadai basi serikali italazimika kulipa bn 600!! Bila kujali mfuko utakuwa na kiasi gani na walioiba wamerejesha kiasi gani, na kwenye kilimo zimeenda kiasi gani..

  Hivyo basi kwenye kilimo zitaenda zile bn 100 zitakazokuwa zimerejeshwa lakini serikali itayalipa makampuni hayo bn 600!. Halafu mwanaCCM mwenzangu unaandamana kuunga mkono jambo hilo.

  Kilichofichwa hapa ni kwamba makampuni feki yaliyoba fedha za EPA imeshasemwa mara nyingi kuwa yalitumia sehemu ya fedha hizo kwenye kampeni za CCM na ndiyo maana wao wako tayari kurudisha kile walichotumia wao lakini hawawezi kurejesha kile walichoipa CCM. Kwa kuwa CCM haiko tayari kurejesha fedha hizo, basi kimantiki na wao hawako tayari kuzirejesha. Ndiyo maana hadi sasa hatujaambiwa nani amerudisha kiasi gani na kimewekwa wapi. Waziri wa fedha alipotangaza kuwa bn 60 zimerejeshwa, aliishia hapo, maana maswali yalizidi majibu..

  Sasa serikali inatafuta mbinu ya kulipa fedha hizo kwa wanaodai; ndipo inakuja na mazingaombwe haya kwamba fedha hizi ziingizwe kwenye kilimo (ili wakulima wafurahi na kushangilia) na baadae ianze kulipa kwa kisingizio kuwa fedha zilitumika kwenye kilimo!

  Tunataka takwimu sahihi na zithibitishwe na chombo kisichoegemea upande wowote kama CAG :-
  Mfuko wa EPA ulipokea fedha kiasi gani?
  Hivi sasa zipo kiasi gani
  Tofauti ielezwe imekwenda wapi, kama ndiyo hiyo ilifisadiwa basi tujue kikamilifu kiasi hicho
  Fedha zitakazorejeshwa ijulikane nani karejesha nini na lini na nani kazipokea.
  Zitakazoenda kwenye Kilimo zijulikane ni kiasi gani na kama ni zile zilizorejeshwa au ni baki iliyo kenye mfuko hivi sasa?

  Mwisho tujiulize rais anayo mamlaka ya kuzuia mtuhumiwa asifikishwe mbele ya sheria? Kama anayo mamlaka hayo, ni sheria ipi, maana katiba imempa uwezo wa kusamehe wale waliokwisha hukumiwa. Je kwa rais kuzuia wasishtakiwe eti kwa kuwa watakuwa wamelipa havunji katiba? Je rais akivunja katiba aliyoapa kuilinda, ni htua zipi zichuliwe dhidi yake?
   
 2. w

  wajinga Senior Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kamakabuzi hongera. Hivi watanzania hawawezi kuchukua class action ya hii kitu tafadhali saidia.
   
Loading...