Mie sishangai kwa wao kusihiwa hoja, lazima wamuogope......pata picha J.K mojawapo ya hoja zake ni kuwa amewaletea maisha bora watanzania kwa sabaabu ya foleni za magari DSM, real president? VIVA MPIGANAJI SLAA
Alitoa kauli hiyo tarehe 19 July 2010 wakati akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Rais Kikwete kuchaguliwa kuwa mgombea pekee wa urais kwa asilimia 99.16, Dkt. Ali Mohammed Shein kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais Zanzibar na Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais
Majibu yangu kwa J.K …………."Magari mengi si ya watu binafsi, idara nyingi za serikali ziko hapa, kuanzia ikulu, bunge, wizara zote, taasisi binafsi, mashirika ya dini, viwanda na wafanyabiashara mbalimbali ambao ndio wamiliki wa magari, sio wananchi wa kawaida, sasa huwezi kusema kuwepo kwa foleni za magari ya idara hizi ni maisha bora kwa wananchi,"