JK na dhana ya kama mkate haupo si wale keki

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Katika hotuba yake ambayo hivi sasa inafikia ukingoni. JK amejikita zaidi katika kueleza mafanikio ya serikali yake. Kwa mwananchi wa kawaida baadhi ya mafanikio hayo anayojivunia yanatia kichefuchefu; kwa mfano amesema ya kwamba serikali yake imefanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei hadi kufikia asilimia 5. Kauli hiyo ukiilinganisha na jinsi mambo yalivyo huko sokoni inadhihilisha kuwa kweli JK yuko katika dunia yake; maana tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita bei za bidhaa nyingi zinazotumika na watu wengi zimeongezeka maradufu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom