JK: Hakuna Ujamaa tena Tanzania

JK: Hakuna Ujamaa tena Tanzania

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2010
Posts
1,007
Reaction score
601
Rais Kikwete hatimaye amekomesha kigugumizi cha Viongozi wengi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakishindwa kutamka waziwazi hadharani kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa siyo nchi inayoongozwa na sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Ingawa kwa miaka mingi Ujamaa umezikwa katika nchi yetu, bado Katiba ya nchi imeendelea kutamka kuwa nchi yetu ni ya Ujamaa. Alipokuwa akizungumza na wazee wa Dar hapo jana, uzalendo ulimshinda JK na akatamka waziwazi kwamba anapokwenda nje kutafuta wawekezaji huwa anawaambia,"Ujamaa haupo siku hizi Tanzania", hivyo hakuna tena masuala ya kutaifisha mali za wawekezaji.
 
Maana yake ni kwamba bla bla za "rushwa ni adui wa haki" na masuala yote ya kukemea ubadhirifu wa mali za umma, siyo dili tena. Chukua Chako Mapema, ndiyo sera rasmi sasa!
 
Gumegume,

Hapo kwenye nyekundu ...inabidi uwe mwangalifu usichukue za madafu! Chukua za wakubwa tunaowategemea

Maana yake ni kwamba bla bla za "rushwa ni adui wa haki" na masuala yote ya kukemea ubadhirifu wa mali za umma, siyo dili tena. Chukua Chako Mapema, ndiyo sera rasmi sasa!
 
Rais Kikwete hatimaye amekomesha kigugumizi cha Viongozi wengi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakishindwa kutamka waziwazi hadharani kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa siyo nchi inayoongozwa na sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Ingawa kwa miaka mingi Ujamaa umezikwa katika nchi yetu, bado Katiba ya nchi imeendelea kutamka kuwa nchi yetu ni ya Ujamaa. Alipokuwa akizungumza na wazee wa Dar hapo jana, uzalendo ulimshinda JK na akatamka waziwazi kwamba anapokwenda nje kutafuta wawekezaji huwa anawaambia,"Ujamaa haupo siku hizi Tanzania", hivyo hakuna tena masuala ya kutaifisha mali za wawekezaji.

Kwahiyo they are EXPLOITING people in the RURAL AREAS... kwa kutumia NGUVU zao Dictatorial; kuwaambia wajenge Ofisi za CHAMA; Hospitali; Barabara wakati kama sio SERIKALI ya Ki-SOCIALIST wangetakiwa kuwa wanalipwa Hourly

Sasa ina Maana Wanapokwenda CHINA ni kuiuza NCHI YETU tu na sio kufuata hizo ITIKADI kama zamani... ??

every One should CRY FOR OUR BELOVED COUNTRY - hatujui tunapelekwa wapi na kwa Mantiki GANI
 
Sasa imekuwa rasmi kuwa siasa ya Ujamaa na kujitegemea, imeuawa rasmi na JK jana wakati anawahutubia wazee wa Darisalama.

Kumbe sasa tumeelewa kiini cha Presidaa wetu kuwa siku zote kuwa kiguu na njia, kutembelea nchi wahisani, kutembeza ' bakuri'

Kumbe safari hizo zina mantiki kubwa, kwa sababu kumbe nchi yetu haina tena ile siasa ya kutaka kujitegemea yenyewe!

Bali ina sera ya kuendelea kuwa omba omba, hadi siku ya mwisho wa dunia hii!
 
Hata mimi nilishangaa sana hili jambo kutamkwa na rais kwa sababu katiba yetu bado inatambua nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea.

Lakini hata hivyo nafikiri ameona awe wazi kuliko kuwa mnafiki.
 
Back
Top Bottom