JK awaita mawaziri wote Dodoma leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK awaita mawaziri wote Dodoma leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, May 24, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni Habari katika gazeti la Mwananchi leo

  Mawaziri wote waitwa Dodoma

  Ramadhan Semtawa
  SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza jipya la Mawaziri, mawaziri wote wameitwa mjini Dodoma, huku taarifa zikisema pamoja na mambo mengine, wanatarajiwa kujadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13.

  Tangu Rais alipotangaza Baraza hilo Mei 4, mwaka huu timu hiyo nzima haijawahi kukutana na hicho ni kikao cha kwanza kwa mawaziri wote chini ya uenyekiti wa mkuu huyo wa nchi.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amethibitisha kuwepo kwa kikao hicho akisema ni cha kwanza tangu kuteuliwa kwao.

  “Ni kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri. Ndiyo ni cha kwanza kwani tangu kuteuliwa kwa mawaziri hakuna kikao ambacho kimewahi kufanyika. Ni cha kawaida tu katika utendaji kazi wa baraza,” alisema Balozi Sefue.

  Habari zaidi zinasema kuwa karibu mawaziri wote waliondoka jana kuelekea Dodoma kwa ajili ya kikao hicho ambacho kinafanyika kabla ya kuanza kwa Bunge la Bajeti mnamo Juni 12, mwaka huu.

  “Wapo ambao wanaweza wakawa Dar es Salaam au nje kwa kazi maalumu. Hawa wanaweza kupata kibali cha Waziri Mkuu. Lakini, karibu mawaziri wote waliondoka jana kuelekea Dodoma,” kilidokeza chanzo kingine.

  MY Take: Ikumbukwe ma RC na Ma DC wote na Ma RAS wote pia wako Dodoma. Hii ni aina ya kuwaongeza mawaziri hawa katika semina elekezi inayoendelea huko. Lakini serikali haina pesa za kulipa mshahara watumishi wake kwa wakati.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,494
  Trophy Points: 280
  Wanajadili bajeti zilizojaa usanii!!!!? Bajeti ya mwaka 2010/2011 ilikatika December 2010 na Serikali ikawa na ukata wa kutisha hadi ikaanza kupitisha bakuli kwa nchi wafadhili...Iliyofuata ya mwaka 2011/2012 ilikatika August 2011 hatimaye November 2011 Serikali ikakiri hadharani kwamba ina ukata wa kutisha....sijui hii bajeti ijayo ya 2012/2013 itadumu kwa muda gani!? Na hili la uchumi wa nchi za wafadhili hasa European countries kusuasua halisaidii hata kidogo.
   
 3. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wanajadili au wanfundishwa namna ya kudanganya na kufukia mashimo ya ahadi zao.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hii ni semina elekezi tu.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Siko optimistic na chochote hapo
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  moja ya sababu ambazo rais anaweza kuachia madaraka ni pamoja na ugonjwa au kifo..
   
 7. d

  dada jane JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmh unamaanisha nini.
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Inavyoonekana anayehitaji semina elekezi ni JK mwenyewe.
   
 9. U

  Uswe JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  umaanisha nini unaposema budget ilikatika, au ni muhimu kuulizana kwanza budget ni nini?
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  budget ni nini????
   
 11. Chigwiyemisi

  Chigwiyemisi JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 531
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Anamaanisha kwamba rais ni mgonjwa kwa hiyo aachie ngazi..
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Labda wanataka kukumbuka shuka ingali kumekucha!  Tuwamwage mafisadi tuwamwage*2 Tuwamwageeeeeeeeeeeee!!
   
 13. B

  BigMan JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  hakuna cha ajabu kwa kocha kuita wachezaji wake kambini,tumekusa cha kujadili
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tangu JK aingie madarakani mwaka 2005 ameendesha semina elekezi kadhaa kwa viongozi na watendaji waandamizi wa Serikali lakini sioni kama semina hizo zinaleta tija yoyote kwa mustakabali wa Taifa letu mbali na kuongeza gharama za uendeshaji pekee.

  Kwangu mimi naona semina elekezi kama moja ya madirisha yanayotumiwa na watawala kutolea fedha za walipakodi kwa faida yao binafsi na sio Taifa letu.
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mbona Sefue Kajadili? basi Jadili hiyo habari nyingine ya Ugonjwa na Urais hapo juu.
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hamna jipya yote ni yale yale jinsi ya kuitetea bajeti ijayo
   
 17. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ni kawaida kabisa kiongozi kuita watendaji wake,iwe kitaifa,kimkoa,kiwilaya na hata kwenye halmashauri.ni jambo la kawaida kabisa.
   
 18. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Vingi ya vikao ambavyo vimefanyika mpaka sasa, hakuna hata kimoja ambacho kimeonesha kuwa na tija zaidizaidi ni matumizi mabaya ya pesa. Tumeshashuhudia semina elekezi Dodoma na Ngurudoto, mwisho wa yote imekuwa ni uvurundaji wa kupitiliza na hata hao mamlaka za usimamizi wao wamekuwa hawana sauti za kuwaadabisha, zaidizaidi wamekuwa wakiishia kulalamika kama sio watu wenye mamlaka. To hell with semina elekezi!
   
Loading...