JK anasimamia vyema mchakato wa Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK anasimamia vyema mchakato wa Katiba mpya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by sumasuma, Feb 8, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TUMEGUSWA sana na jinsi Rais Jakaya Kikwete anavyosimamia vyema mchakato wa kuwapatia Watanzania Katiba mpya. Siyo siri kuwa, mchakato huo ulipoanzishwa mwaka jana, wakosoaji wengi walisema walikuwa na mashaka kama kweli Rais Kikwete alikuwa na nia ya dhati alipotangaza kwamba angehakikisha nchi yetu inakuwa na Katiba mpya ifikapo mwaka 2014 na kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

  Mashaka ya wakosoaji hao bila shaka yalitokana na utamaduni uliozoeleka katika nchi nyingi za Afrika, ikiwamo Tanzania ambapo maamuzi mengi yanayofanywa na viongozi wa serikali hizo aghalabu hufanyika kisiasa kwa lengo la kuvinufaisha vyama tawala na kuvidhoofisha vyama pinzani. Ndiyo maana wananchi wengi awali waliamini kwamba Rais Kikwete kwa vyovyote vile asingesimamia upatikanaji wa Katiba mpya iliyopatikana kwa maridhiano na mwafaka wa kitaifa.

  Lakini Rais Kikwete amewashangaza watu wengi, wakiwamo wanachama na wafuasi wa chama chake cha CCM, kwa msimamo wake wa kutaka ipatikane Katiba mwafaka iliyoridhiwa na wananchi wote. Pamoja na Rais kutia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, ambayo ilipitishwa kishabiki bungeni kwa wingi wa wabunge wa chama chake cha CCM, bado baadaye alikutana na viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu na kukubaliana nao kuhusu baadhi ya vipengele katika sheria hiyo ambavyo vinahitaji kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya taifa.

  Muswada wa marekebisho hayo jana ulikuwa ujadiliwe na Bunge linaloendelea na mkutano wake wa sita mjini Dodoma, lakini uliondolewa ghafla katika orodha ya shughuli za Bunge baada ya wabunge wa CCM kutishia kuukataa kwa madai kwamba marekebisho ya sheria hiyo yangekiweka chama chao kitanzini na kukipa Chadema nguvu kubwa ya kisiasa.

  Pengine ni vyema kukumbuka kuwa, Chadema ilisusia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba mwaka jana baada ya kuona hoja zao kuhusu muswada huo zilikuwa zinapuuzwa na wabunge wa chama tawala kwa kutumia wingi wao. Kitendo cha Rais kukutana nao Ikulu na kusikiliza na kukubali hoja zao, hata baada ya kusaini muswada huo kuwa sheria, ndicho hasa kimeibua hasira za wanachama na wabunge wa CCM kiasi cha wabunge hao kuamua kususia kujadili muswada huo na kukataa ombi la Rais aliyetaka kukutana nao jana mjini Dodoma.

  Tunaambiwa kwamba baada ya wabunge hao kukataa ombi hilo, baadaye waliunda timu ya wajumbe watano ili wakutane naye kama Mwenyekiti wa chama hicho. Wajumbe hao walikutana naye, ingawa ni mapema mno kujua Rais alitumia mkakati gani kulainisha msimamo mkali wa wabunge hao, kiasi cha kukubali kuujadili na kuupitisha muswada huo leo. Hata hivyo, zipo duru za kisiasa zinazosema Rais aliwaambia wabunge hao kwamba alikubali hoja za Chadema kwa sababu aliona siyo tu zilikuwa zinaboresha sheria hiyo, bali pia zilikuwa zinazingatia maslahi ya taifa. Aliwataka wapime madhara ya kuyakataa marekebisho hayo na faida na manufaa ya kuyakubali kwa maana ya kupata maridhiano na mwafaka wa kitaifa katika kuandika Katiba mpya.

  Safu hii pengine siyo mahala stahiki pa kuorodhesha hoja zote za Chadema au vyama vingine vya siasa ambazo zilikubaliwa na Rais na kuingizwa katika muswada wa marekebisho ya sheria hiyo. Hata hivyo, tunampongeza Rais kwa kusimama kidete kulinda maslahi na umoja wa taifa letu pasipo kutetereka ama kuyumbishwa na siasa za itikadi za vyama. Tunampongeza pia kwa kutambua kwamba Katiba ya nchi ndiyo sheria mama ambayo kwayo ndiyo dira inayoongoza shughuli za mamlaka zote, ikiwamo mihimili mitatu ya dola hivyo, katiba hiyo itakuwa halali pale tu wananchi wote watakaposhirikishwa katika mchakato wote wa kuipata.

  Tunawashauri wabunge wote leo waonyeshe uzalendo kwa kuyapitisha marekebisho ya sheria hiyo, hata kama mitima yao imekwazwa kiasi fulani na hatua ya Rais ya kukataa kupitisha ongezeko la posho zao za vikao.
  :shock:
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  sasa "MNAPONGEZA" wewe na nani mnaempongeza?? "TUNAAMBIWA".. watu wengine bwana

  au nyie ndio kile kikundi mlichopanga kum-assasinate wakati wa uhuru??
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kitendo cha kukutana na wapinzani ikulu na kuwasikiliza na kufanya marekebisho ya sheria ni mwanzo mzuri. Hatua hii inatia moyo.
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tumpongeze JK kwa hatua alizokwishachukua na ambazo ataendelea kuchukua ikiwa ni pamoja na kukubali marekebisho ya uteuzi wa wajumbe wa tume ya kukusanya maoni.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tuanze kumtajia wajumbe wa Tume ya Katiba:
  -SAS- Mwenyekiti.
  -Dr AS Migiro- Makamu
  -Mabere Marando- Katibu
  -Jenerali Ulimwengu- Mjumbe
  -Helen Kijo Bisimba-Mjumbe
  -MzeeMwanakijiji- Mjumbe
  -Mchambuzi- Mjumbe
  -etc. nk.
   
Loading...