Rais Kikwete ametoa utabiri huo wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM huko mkoani Mbeya. Alisema kwamba chama kimekithiri kwa ufisadi, dhuluma, rushwa, hongo, umangimeza na vitendo vingi vichafu suala ambalo linapunguza imani ya wananchi kwa chama na serikali.
JK alionya kwamba endapo chama hakitachukua hatua za makusudi kujisafisha, hakitavuka 2015 na akawatahadhalisha wanachama wake kujiandaa kisaikolojia kuchukua nafasi ya chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi wa mwaka 2015--kwa kuwa haoni dalili za chama kujirekebisha na kurejesha mvuto kwa watanzania kabla ya uchaguzi ujao.
Akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya BBC leo asubuhi, kada maarufu wa CCM na ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya madini, Bw Richard Kasesela, alikiri kwamba sasa hivi CCM ni kama gulio--mwenye pesa ndiye anayenunua uongozi. 'Watu wanatembeza pesa makanisani na misikitini mchana kweupe bila kuhojiwa wamezipataje hizo fedha', alihoji Bw Kasesela.
MY TAKE:
Ni afadhali wanaCCM mmeamua kusema ukweli. Vzr sana!