JK abanwa mbavu; Ujumbe wa bajeti yake ni madeni matupu, ahadi hewa na haitekelezeki

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

picture-9.jpg

Na Alfred Lucas - Imechapwa 20 June 2012



RAIS Jakaya Kikwete amepelekewa ujumbe kwamba bajeti ya serikali yake "ni ya madeni matupu, ahadi hewa na haitekelezeki," MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Hili limewekwa wazi katika hotuba za baadhi ya wanasiasa – hasa wabunge, katika mahojiano na wataalamu wa uchumi, wafanyabiashara na wananchi.


Bajeti ambayo ilitangazwa Alhamisi iliyopita bungeni mjini Dodoma, imeelezwa kuwa haina jipya; wengine wakisema "…ni yaleyale ya mwaka jana, mwaka juzi."


Msingi mkuu wa baadhi ya wabunge na waliohojiwa kuikataa bajeti ya 15 trilioni, ni taarifa kwamba serikali ilishindwa kutekeleza bajeti ya mwaka jana kama ilivyopendekeza bungeni.


Serikali yenyewe imekiri kutofanikisha ahadi zake na mipango yake; ikiwa ni pamoja na kutopeleka kwa wakati mwafaka au kutopeleka kabisa fedha ilizoahidi idara, wizara na halmashauri.


Katika baadhi ya wilaya, viongozi wamekiri kupokea chini ya asilimia 40 ya fedha walizoahidiwa.


Wakati serikali ilishindwa "kupata" fedha kwa mipango yake, imekiri pia kuwa baadhi ya misaada na mikopo ya kibiashara kutoka nje haikufika kwa wakati na mingine haikupatikana kabisa.


Juu ya ahadi na mipango ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2011/12 ambayo haikutekelezwa, mwaka huu, serikali imeendeleza baadhi ya mipango na kuahidi mipango mipya.


Mipango hiyo ni pamoja na kilimo kikubwa cha miwa na ujenzi wa viwanda vya kutengeneza sukari.


Wasiwasi wa wananchi na wataalamu umeelezwa kuwa kama serikali ilishindwa kukusanya fedha za kutosha bajeti iliyopita, itawezaje kufanikiwa mwaka huu.


Kinachojadiliwa zaidi ni takwimu zinazoonyesha kuwa serikali inatumia fedha nyingi kuliko inazokusanya kwa njia ya kodi.


Lakini kilichoongeza wasiwasi zaidi juzi Jumatatu, ni taarifa kwamba wizara nne hazijakamilisha bajeti zao kutokana na kamati za kudumnu za bunge zinazohusika, kuamuru marekebisho katika maeneo mbalimbali.


Hata hivyo, tayari baadhi ya kampuni zimeanza kulalamikia kodi waliyowekewa na serikali kuwa ni kubwa mno na "itaathiri uzalishaji."


Kampuni mbili ambazo zimefahamika kuonyesha kutoridhika na kiwango cha kodi kilichowekwa na serikali zimetajwa kuwa ni Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kampuni ya Bia (TBL).


Imeelezwa kuwa mapema mwaka huu, kampuni hizi ziliandikia serikali (wizara ya fedha) zikiomba kuwa iwapo serikali itaamua kuongeza ushuru wa bidhaa zao, basi ongezeko lisizidi kiwango cha asilimia 10.


Hoja ya kampuni hizo haikukubaliwa. Mawasiliano ya TCC ambayo MwanaHALISI limeona yanalalamikia kikosikazi (task force) juu ya hatua za mabadiliko katika kodi, kuwa hakikuonyesha ushirikiano kwa sekta binafsi.


Mawasiliano hayo yanasema, pamoja na mambo mengine, "…katika mazingira ya mfumuko wa bei wa asilimia 19, kuongeza kodi kwa asilimia 19 au kwa zaidi ya asilimia 10 tu, kutapotezea serikali mapato badala ya kuiongezea."


Taarifa hiyo ya TCC kwa serikali iliambatanisha takwimu kuonyesha jinsi serikali itakavyoshindwa kupata mapato iliyoyatarajia.


Katika andishi jingine la TCC ambalo gazeti hili imeliona, kampuni inasema kiwango cha kodi kilichopitishwa cha asilimia 18.7, "…kitadhuru biashara yetu kwa kiwango kikubwa."


Aliyeandika andishi hilo anasema aliwahi kukutana na wajumbe watatu wa kamati ya magwiji ya bajeti (David Tarimo, Profesa Wangwe na Mama Kilindu) na kuwaomba kumshauri waziri juu ya suala hilo.


Katika hatua nyingine, anasema, "Huko nyuma, kuingilia kwa mwenyekiti wa TBL, Cleopa Msuya kuliongeza uzito." Hata hivyo, hawakufanikiwa kuishawishi serikali.


Nao TBL wanaeleza namna walivyofanya mawasiliano na serikali kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kodi yasivuke asilia 10.


Andishi lao linasema wanaelewa kuwa sheria inaruhusu marekebisho ya kodi kuwiana na viwango vya mfumuko wa bei; lakini linasema hiyo ilikuwa wakati mfumuko ukiwa chini ya asilimia 10.


"Tuna uzoefu wa Zambia ambako serikali ilizidi kuongeza kodi ya bia kiasi cha kufanya viwango vya uzalishaji kupungua na kusababisha serikali kukosa mapato iliyoyahitaji," limeeleza andishi.


Ongezeko la kodi kwa viwango hivyo, amesema ofisa mmoja wa TBL, "Litasababisha kupungua kwa uzalishaji, makusanyo ya kodi, uwezo wetu wa kununua malighafi na pia kuathiri shughuli za viwanda vinginevyo na wakulima wetu wa mtama na shayiri."


Amesema, "Pasipo shaka, ajira zetu na washiriki wetu wengine wa kibiashara zipo hatarini; na pia miradi mingine ya uwekezaji itabidi iangaliwe upya kwani hali hii ya sasa haiwezi kutoa taswira inayohalalisha uwekezaji zaidi hapa nchini katika viwanda vyetu."


Bajeti ni sheria ya mapato na matumizi, inayotungwa kila mwaka kuelekeza jinsi ya kukusanya mapato na kusimamia utekelezaji wa mipango kama ilivyoainishwa na serikali.


Mwaka huu, serikali imepanga kutumia Sh. 15 trilioni kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Bajeti ya mwaka jana ilikuwa Sh. 13 trilioni.


CHADEMA yapigilia msumari



  • Serikali imeshindwa kutekeleza bajeti inayokwisha (2011/2012) na hata ahadi walizotoa za kupeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo hazikutimizwa.



  • Serikali ya CCM imekataa kuchukua mapendekezo ya upinzani ya kuongeza na kuimarisha ukusanyaji mapato.



  • Bajeti imekuwa ya mjini zaidi na haikuzingatia wananchi wa vijijini.



  • Serikali imeshindwa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira.



  • Imeshindwa kusimamia kwa tija mpango wa elimu vyuo vikuu na hatimaye kusababisha migogoro ya mara kwa mara.



  • CHADEMA itarekebisha sheria za kodi katika eneo la madini na simu.



  • Kutunga sheria za kusimamia mikopo kwa kampuni za wawekezaji ili isizidi asilima 70 ya fedha zilizowekezwa.



  • Mauziano ya kampuni yenye mali zake nchini yatozwe kodi asilimia 30.



  • Misamaha ya kodi isivuke asilima moja ya pato la taifa na ipitishwe na kamati ya fedha na uchumi ya bunge.




 
Tuna Madini kwanini tusiwaambie hao wanayoyachimba sasa tunataka Asilimia 10% au 20% kulipia Budget yetu?

Kuliko kutegemea BIA na SODA? Kwanini Tusimuombe Mtukufu Rais aache hizo Safari za Nche na Umati wa Watu

Bila Sababu? Wapiga Pasi 3 hiyo ilikuwa Trip ya Rio; Wakati katika Hoteli zote za Grade A zina Wapiga Pasi bora

Zaidi ya hao anaowabeba toka Bongo?
 
Hali tumia muda mwingi kushindana na serikali ya awamu ya 3 na kutafuna pesa alizo kusanya mkapa, sasa yake inamshidwa. Sawa si mlichagua sura? Hali ya maishi ni tete sabuni juu, mafuta taa juu, sukari juu. Kweli nimeamini tabasamu lake uhashiria udhaifu wake. Soma kitabu cha man of the people utapata jibu.
 
Back
Top Bottom