Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Wanajamvi: Hii imekaaje? rais atoa agizo la kuwauwa majangili? Huu kweli ni utawala wa sheria? Au amenukuliwa vibaya na gazeti hilo la RA?
Rais jakaya kikwete ameagiza wizara ya maliasili na Utalii iwadhibiti majangiliu katika hifadhi za taifa, na ikibidi kuwauwa.
Rais Kikwete akitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika wizara hiyo juzi (Jumanne) ambako pamoja na mambo mengine, alionyesha kukerwa na ujangili (poaching) nchini……..
Habari zaidi katika Mtanzania ya leo (Friday).
...Wiki iliyopita Pinda, akiwa ziarani mkoani Tabora, alisema wanaothibitika kuua albino nao wauawe kwa kuwa hakuna sababu ya kuwapeleka polisi wakati wanakamatwa wakiwa na viungo vya albino pamoja na damu kuashiria wameshiriki mauaji hayo.
Source: Tanzania Daima 30/01/2009
Naomba niendel off topic kidogo
Majangiri sio watu na ni vizuri wauwawe, hakua cha utawala wa sheria wala nini!!!
Hamkumbuki kwamba Bunge letu TUKUFU lilishapitisha sheria ya kuua watu wanokutwa kwenye mbuga za wanyama?