Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,080
- 79,478
JITOFAUTISHE NA WENGINE
Na, Robert Heriel
Katika maisha ogopa na usitake kufanana na mtu mwingine. Ogopa kuiga, usiige maisha, jitofautishe na wengine. Ili maisha yawe magumu yanahitaji jambo moja tuu, kuiga, ili maisha yawe rahisi sana yanahitaji jambo moja tuu, KUJITOFAUTISHA NA WENGINE.
Watawala wa dunia na watu wenye akili wanajua kanuni hii, na wanatumia nguvu kubwa kuwafanya watu wafanane kwani katika kufanana ndipo ilipobiashara. Ndio maana kuna mambo ya fashion katika kila jambo iwe mavazi, vyakula, vinywaji, mitindo ya ujenzi wa makazi, siasa na sheria za nchi, simu, magari miongoni mwa mambo mengine.
Hivyo hutumia propaganda nyingi kuwafanya watu wengi hasa walio na akili nyepesi, kuingia kingi na kujiona duni kuwa kama wasipoendana na dunia basi wamefeli maisha.
Usishangae vijana wakihangaika kuvaa vizuri kuendana na mitindo ya kidunia, usishangae watu wakihangaika kununua magari, simu kali ili waendane na kasi ya dunia, na wasipofanya hivyo huonekana washamba au watu waliopitwa na wakati.
Lazima Ieleweke kwamba, kuendana na dunia sio kufanikiwa bali ni kuwa mtumwa wa watu wengine, hasa wale wanaoamua dunia iendeje.
Nashaurigi vijana kuwa, kuiga ni jambo zuri kama utaiga kwa asilimia ndogo sana, kama utaiga basi isizidi asilimia ishirini na tano 25%.Kama mtazamo wako utauweka kwamba unaishi maisha yako kwa asilimia 80% kisha utaishi maisha ya watu wengine yaani utaiga kwa 20% basi upo katika hatua nzuri ya kufurahia maisha, na kufanikiwa kwa jambo lolote unalolitaka.
Baada ya haya tuje kwenye kiini cha mada yetu, Kisemacho; JITOFAUTISHE NA WENGINE katika mtazamo wa kimajumui.
Usijione bora kuliko wengine bali fanya mambo bora mpaka uonekane bora na watu wengine. Usipende kusifiwa bali jisifu kwa yale bora uyafanyayo. Usikubali kusifiwa sifiwa, jisifu wewe mwenyewe kwani wewe ndio unajijua uwezo wako. wanaokusifu hawakujui, wanakukadiria tuu kwa kile ulichokifanya.
Unapoenda kanisani au msikitini kusali, unapofunga na kuomba, jitofautishe na ambaye haendi msikitini au kanisani, jitofautishe na ambaye hafungaji wala haombaji. Hakikisha unamzidi katika kile unachokifanya. Sio unaenda kanisani sijui msikitini kusali, unamuomba Mungu akupe maisha mazuri alafu unalingana maisha au kushindwa maisha na mtu ambaye haendi msikitini wala kanisani. huo ni upumbavu, huko ni kujichoresha na kuaibisha kanisa au msikiti au huyo Mungu unayemuomba.
Mimi huwaga nawaambia watu hivi, siendi kanisani bure, sifungagi bure, yaani uende kanisani kila siku, ufunge kila wiki, uombe Mungu kila muda alafu ulingane jambo fulani na asiyeomba huo ni upuuzi, kupoteza muda na kujichoresha.
Kama sio kumuabisha Mungu wako, labda awe mungu mshenzi ambaye hana lolote lile.
Ukienda kanisani au msikitini jitofautishe na wasioenda, hakikisha unakuwa mfano bora kwa jamii, sio unaenda kanisani alafu unakuwa njaa njaa, omba omba, huna lolote, unashindwa hata na wasioenda kanisani au msikitini. Huo ni upumbavu.
Usifanye jina la Mungu wako likatukanwa kipumbavu pumbavu.
Ati unaenda kanisani au msikitini alafu unamuomba msaada asiyeenda, wewe kama sio mpuuzi ni nani. Jitofautishe na watu wengine, uache upuuzi.
Usikubali kufanya jambo lolote bure, usikubali kupoteza muda wako bure. Ukiwa wa Mungu jionyeshe kama wa Mungu, unashindwaje na watu waovu. Sisemi uwe na utajiri wa kutisha hasha! nazungumzia maisha ya kawaida yasikushinde.
Huwezi ukamuabudu Mungu wa kweli alafu ukawa njaa njaa, huo ni uongo wa mchana, yaani ufuate maagizo yake na maelekezo yake yote alafu uwe sawa na asiyefuata hiyo sio kweli. Huwezi ukamtegemea Mungu ukawa njaa njaa, narudia kwa msisitizo. Ukiona unamtegemea Mungu alafu unakuwa njaa njaa basi jua kuwa huyo mungu wako niwa makaratasi, na kama ni wakweli basi hufuati maagizo yake isipokuwa unajidanganya au kudanganya watu wakuone mtu wa swala sana kumbe mnafiki.
Jitofautishe na watu wengine.
Haiwezekani mtu usome alafu ufeli, sijawahi kuona popote pale. Ukisoma lazima ufaulu darasani, hiyo ni lazima. Ukiona mtu alikuwa msongokaji darasani alafu akafeli basi jua alikuwa anawaongopea wenzake. Na ukiona mtu amefaulu mitihani ya darasani alafu ulikuwa humuoni akisoma soma basi jua kuwa alikuwa na muda wake maalumu wa kusoma hata kama ni muda mchache. Huwezi kufaulu bila kusoma huo ndio ukweli.
Kama umesoma, Jitofautishe na asiyesoma, haiwezekani mtu usome miaka nenda rudi alafu ufanane na ambaye hajasoma, wewe ni popoma kama upo hivyo. Yaani utumie zaidi ya miaka kumi na sita kusoma tuu alafu ulingane na mtu ambaye hajasoma au ametumia miaka minne au saba, wewe kama sio mwehu ni nani. Jitofautishe na wengine.
Jitofautishe na wengine kiakili, kimawazo, kimtazamo, kilugha, kimavazi, kiutafutaji wa mali, kimitindo ya maisha, sio unakuwa kama jinga jinga tuu.
Unakuta mtu ni profesa lakini anayoyaongea kama darasa la saba. Jitu limesoma mpaka Degree alafu hana tofauti na ambaye ameishia darasa la saba. Wewe ni mwehu.
Jitofautishe na watu wengine, acha kujidhalilisha kwa upumbavu wako. Wewe unashindwaje na mtu ambaye umemzidi jambo fulani kama sio uzembe na upopoma wako.
Jitofautishe...!
Mtu umeoa au umeolewa, ishi kama mwanandoa, ongea kama mwanandoa, vaa kama mwanandoa, tembea kama mwanandoa, kula kama mwanandoa.
Sio umeoa au umeolewa alafu unaishi kama mtu ambaye hajaolewa au hajaoa.
Unakuta limwanamke limeolewa lakini ni jinga haijapata kutokea, linavaa nguo za hovyo, limwanamke limeolewa lakini ni malaya, linalala na wanaume kama mbwa, yaani kila dume anataka limpande. Jitofautishe. Jiheshimu kama mke wa mtu. Heshimu mume wako, heshimu watoto wako. Jiheshimu kama mke mwema.
Unakuta mwanaume ameoa lakini ni mpuuzi hujapata kuona, linatapanya pesa nje huku likishindwa kulea mke na watoto.Mwanaume hajiheshimu kazi kugonga wanawake wa nje na kuzaazaa hovyo kama mbwa. Jitofautishe na ambao hawajaoa.
Kama ulitaka ufanye upuuzi wako usingeoa au kuolewa, ungefanya ukahaba wako na uasherati wako mpaka uchoke. Sio uoe au kuolewa alafu ulete upopoma wako ndani ya ndoa.
Jitofautishe,,,
Mtu unafanya kazi lakini hauna tofauti na asiyefanya kazi. Usipende kufanya kazi bure, jitofautishe na wasiofanya kazi. Fanya maendeleo, vaa vizuri, kula vizuri. Sio unafanya kazi miaka nenda rudi alafu huna lolote yaani huna tofauti na ambaye alikuwa hafanyi kazi. Huo ni upuuzi.
Jitofautishe...
Kama ni mwanaume hakikisha unajitofautisha na mwanamke. Usiwe na mambo ya kike, fanya kama mwanaume, Ongea kama mwanaume, tembea kama mwanaume, vaa kama mwanaume. Sio umezaliwa mwanaume alafu unaleta mambo ya kiduwanzi.
Kama ni mwanamke, hakikisha unajitofautisha na mwanaume. Usiwe na mambo ya kiume, fanya kama mwanamke, ongea kama mwanamke, deka, mikogo, ringa, jirembe, vaa kama mwanamke. Sio umezaliwa mwanamke alafu unaleta pigo za kidume, huo ni upopompo.
Jitofautishe na wengine.
Taikon nimemaliza, mwenye swali anaweza kuuliza.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Morogoro Mjini