Jitihada zote za Kinana za kujenga chama zinaangushwa na serikali yake

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,646
1,168
Katika watu ambao ni wanasiasa wa kweli hapa nchini kinana ni mmoja wao. Amekuwa akizunguka nchi nzima kuhakikisha upinzani nchini haupati nafasi , wakati yeye akizunguka na wapinzani nao kila siku wapo njiani kuhakikisha kwamba ccm inaondoka midomoni mwa watu kuanzia mijini hadi vijijini.

Matokeo haya ya serikali za mitaa yanatia nguvu kwamba hazitapita chaguzi tatu mbele ccm watakuwa wameondoshwa madaraka na wananchi. kinachotia faraja ni kwamba upinzani wamepata vitongoji hadi vijijini huko ndani kitu ambacho huwezi kuamini , hii ni ishara kwamba demokrasia inakuwa sasa.

Laiti kama serikali ingekuwa inafuata ushauri wa kinana ccm yasingewakuta haya, kwa sababu kinana anakutana na mengi , anapokea ushauri toka kwa wanachama wa chini kabisa kwa hiyo anajua mengi.

Kwa kuwa ni mpango wa Mungu Kika kinachofanywa na ccm kinaonekana sifuri
 
Mjanja huyo acha ale night zake za mwishomwisho. CCM ni gari iliyochoka hata aje dereva gani litaendelea kusumbua tu. Jamani hili gari kila kukicha matengenezo, uhakika wa safari haupo tena. Mbaya zaidi hata spea zake hazipatikani sasa. Gari lenyewe manual, kila mara linahitaji kusukumwa ili liwake. Nauliza tena KWA NINI TUSINUNUE GARI ZURI JIPYA LA KISASA? HII SCREPA TUMPELEKEE FUNDI KIRA ATENGENEZEE MISUFURIA?
 
Back
Top Bottom