Jitihada za Binadamu Kujiangamiza kwa kutumia akili, maarifa, sayansi na gunduzi mbalimbali ili kujiketekeza

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,268
Katika moja ya tabia ambazo nimekuwa nikipambana nayo ni hii ya kutaka kujua ulimwenguni kumekuwa na nini kikiendelea. Asubuhi sana napoamka najikuta naangalia CNN,BBC,AL JAZEERA,VOA,SKY NEWS,CBN, na local channels kwa habari za kitaifa. Lakini Zaidi Zaidi ni kuangalia channels mbali mbali za gunduzi za kisayansi na historia.

Katika haya yote nimegundua binadamu tunafanya juhudi kubwa sana ya kugundua namna ya kujiangamiza.. kwa marifa mengi,elimu na gunduzi nyingi bado mwishowe hatufanyi maisha kuwa rahisi isipokuwa magumu Zaidi na yenye kuogofya. Tunapambana katika kupambana na sisi wenyewe kuliko kupambana na kila kinachotaka kuangamiza binadamu hapa ulimwenguni.

Ugunduzi na matumizi ya Drones.
Drone.jpg

Kiukweli binafsi huu ni moja ya ugunduzi wenye kuogofya hasa…. Ashakum si matusi kuwa ni kama binadamu kwa sasa “we https://jamii.app/JFUserGuide ourselves” sasa hizi ndege ambazo zinajiendesha zenyewe zimekuwa na uwezo wa kwenda kushambulia kijeshi kwa masafa ya mabli pasipo kuwepo na rubani ndani yake. Ukiangalia kirahisi utasema huu ni ugunduzi wenye manufaa makubwa sana hapa duniani. Lakini kaa fikiria ndege hizi zinaenda kumshambulia nani? Binadamu mwenzetu ..ila zinapunguza madhara kwa anayezituma kwa sababu sasa hazitakuwa na rubani ambaye anaweza dhurika. Lakini je kiuchumi haziathiri nchi husika kutokana na mamilion ya pesa yanayotumika?zina athari yake kubwa tu.

Afrika miaka yote tumejikuta tunaangukia katika makundi makuu mawili… kwa kufuata itikadi,mila na tamaduni husika tunajikuta tukisifia na kuponda upande flani. Lakini swali ambalo kama afrika hatujiulizi maendeleo haya yana tuweka katika mustakabali gani? Nini uelekeo wetu miaka kadhaa ijayo? Afrika tunakuja kutawaliwa. Gunduzi hizi na maendeleo haya tunaweza dhani sisi hayatuhusu na hayana athari kwetu. Lakini tunasahau kuwa hata sasa tunatawaliwa kwa njia moja ama nyingine.

Drones ni kama jini
. Hizi ni ndege majini ambazo zinatumwa kwenda sehemu kufanya uharibifu. Kwa kiwango kikubwa zimekuwa precisely kwa sababu zinaelekezwa ziende wapi na kurudisha feedback kwa kutumia camera ndogo zenye uwezo mkubwa kuhusiana na sehemu husika.hii inazipa uwezo wa kupiga kuua pasipo mhusika kujua nini kimemsibu. Zimeundwa pia na uwezo mkubwa wa kuweza kujificha kuonekana katika rada. Hii ni teknolojia ambao anayekushambulia anakuwa amekaa ofisini anakunywa kahawa huku miguu kapandisha mezani

Maendeleo ya kutisha katika matumizi ya Drones

Kumeendelea kuwepo majaribio ambayo yanaaelekea kuleta mrejesho mzuri juu ya maboresho yanayofanyika.sasa drone inaweza wekewa bunduki ili iwe na uwezo wa kupiga risasi kwa ajili ya kufanya mauaji. Hivyo hii itatumwa kuja kumuua mtu husika…. Ikishafanya mauaji itarudi ilikotoka au hata kama itakamatwa bado aliyeituma hatojulikana na haiwezi kutoa ushahidi.piazimeundwa na uwezo wa kujiipua yenyewe baada ya kufanya shambulio.

Fikiria unatembea sehemu halafu zinakuja risasi kadhaa zinapigwa kutoka kwenye drone. (hakutakuwa tena na haja ya kuwa na watu wasiojulikana kwa ajili ya kazi za mauaji ) Unaanguka na kufa. Na drone yenyewe inalipuka. Basi ….unaokotwa na kuwahishwa hospital.. unafika ukiwa DOA (Dead on Arrival) na kama ulijeruhiwa basi inawezekana bado ukafia njiani kutokana na foleni kubwa zinazotuandama nchi zetu hiz za dunia ya tatu.haya ni maendeleo tunayoyashabikia. tunakoelekea ni hatari zaidi kuliko tulipo.

HARAKATI ZA KUTENGENEZA shambulio la ki EMP

nuclear-war-EMP-attack.jpg

Mfano wa shambulio la kinyuklia la EMP. mfumo wa umeme wote unakuwa hatari na hatimaye kufa na kuua pia.

Unafaham kuwa kuna silaha ambayo imekuwa ikitengenezwa miongo kadhaa ya nyuma ambayo iana kifaa kinachoweza kuzalisha EMP? ( Elecromagnetic pulses) hii inaweza shambulia grid za umeme nchini kwa kuzifanya zikate umeme. Kufanya giza na kutokuwa na umeme kwa nchi nzima kwa kipindi flani.hii inaweza ua mifumo yote ya bank,simu zikafa na computers pia.kila kitu kikavurugika ndani ya muda mfupi tu ukajikuta umeshika Iphone yako ambayo ni useless. mifumo yote ya umeme unauliwa kila aina ya umeme... na tayari Korea kaskazini inasemakana wanalo Bomu kama hili na walitoa Tishio kuwa wanaweza kulitumia dhidi ya USA. ambao wao walishakuwa nalo kwa siri na wakajiongeza zaidi kuanza kutengeneza counter attack yake.fikiria Umepakata Apple yako ambayo ni useless sababu imekufa,mawasiliano yoote kwa njia ya umeme yaathirika huku wenzio wakiwa na uwezo wao kama kawaida tayari kukushambulia.heri kwa wenye tecno hawataumia sana kwa shambulio kama hili.

Unafaham RDD inawezaje kuangamiza binadamu? (Dirty Bomb) bomu chafu

Radio Logical Dispersal Device (RDD) ambayo inakuw ana milipuko iliyopangiliwa kitalam kama vile baruti inaua kwa kupitia mionzi. Kwa kuachia monzi mikali ambayo inaweza sababisha maumivu,mateso na vifo kwa binadamu katika sehemu husika kuliko hata miale inayofahamika kama radioactive. Aina hii ya bomb wenyewe wanaita Dirty Bomb

Robot za Mauaji.
killer robots.jpg

Hizi si Drones. Huu mradi umekuwa ukiendelea kufanyika huko Northrop ,El Sagundo,CA ukifahamika kama X-47b UCAS ( Navy Unamanned Combat Air System Demonstration) au UCAS- D . ni mradi ambao unasimamiwa kwa usiri mkubwa na serikali ya marekani. Inafanana sana na kile ambacho umewahi kukiona kwneye “skynet” hii teknolojia si drones.. ni kitu kingine kabisa. Hii ni mashine ya kuulia. (KILLING MACHINE) hakuna anayekaa sehemu kui control kama ilivyo kwa drones. Ina akili kubwa ya kufanya kile ambacho umeaiambia pasipo tena wewe kuifuatilia na joy stick kama ilivyo kwa drones.ukisha iambia basi inaenda kufanya ulichoiambia pasipo tena wewe kui control na huwezi tena kuiingilia sababu tayari inakuwa imeshafanya maamuzi ya kile ambacho umeiambia.

1. Inajiendesha kwa kujitegemea

2. Inatua na kupaa yenyewe

3. Inaweza kutua kutoka kwenye ardhi au manowari yenyewe

4. Inaweza jijaza mafuta yenyewe

5. Inaweza kuendelea na next target baada ya kumalizana na target ya kwanza
killer robots 2.jpg

Hii ni robot ambayo imeundwa kumuua binadamu. Imeundwa kwa dhamira hiyo na ipo tayari kabisa katika maabara za wenzetu. Hii robot imesimamishwa uzalishaji Zaidi kwa sababu hata walioitengeneza wameshtuka kuwa inafanya kazi kwa ubora kuliko walivyotegemea. Hii ni predator. Project X-47Bs ilifanyiwa majaribio ambayo yaliwaogopesha waliyoitengeza. Kuwa kama ni mtu tungesema imekuwa fit kuliko alivyotegemewa. Imepitiliza.

Mauaji kupitia Virusi hatari Zaidi kwa maisha ya binadamu
spanish-flu-1-25-18-1-1024x623.jpg

watu waliofariki kwa mafua haya wakienda kuzikwa.

Mwaka 1918 kulikuwa na mafua ya Hispania.. . kama sasa tunaposikia habari za mafua ya ndege. Mwaka huo yalikuwepo mafua ya Hispania ambayo yaliua watu kati ya Mill 50- 100. Mafua haya yalisababisha vifor vya watu karibia 70,000 USA peke yake na mwaka 2009 mlipuko kama huo uliua tena watu karibia 284,000. Mwaka 2011 Ron Fouchier na Yoshihiro waliangalia toleo lingine la H5N1 ambalo ni kama Mafua ya Nguruwe na kuchapisha matokeo yake.
fluvictim.jpg

Kifo kibaya cha mateso makali kutokana na mafua haya mwaka 1918 huko Hispania

Hii ilifungua mlango kwa watu wenye kuw ana roho mbaya juu ya binadamu wenzao kuanza kufikiria kutengeneza mabombu ya kikemikali.. kwa miaka mingi iliaminiwa kuwa makundi ya kigaidi hayawezi kuja kupata nafasi au uwezekano wa kumiliki mambo ya hatari kama haya. Lakini ISIS inakadiriwa kuwa na mapato ya karibia USD million 85- 400 na kuwa na umiliki wa vituo kadhaa vya kitabibu. Na inafahamika kuwa Syria imewahi kutumia silaha za kikemikali na wataalamu walioko Syria wanaweza kutumika kutengeneza Virusi hatari kama hao wa Mafua ya Hispania. Hi dunia si sehemu salama tena na ndo maana wenzetu wengine wameshaamua kwenda kuishi sayari nyingine. Unapoangalia Tv series kama The 100 n.k unaweza amini ni mambo ya kufikirika .. lakini kuna kitu ambacho dunia inaambiwa ijiandae nacho. Kuna siku watu watahama hii dunia ,kuna watu wameshajiandalia makazi chini ya ardhi.. kuna watu tutakuja kufutika usoni pa dunia. Binadamu anayafanya haya kwa binadamu mwenzie. Wala si kwa fisi,chui na nyoka.
syria.jpg

Madhara ya silaha za Kibayokemikali huko Syria. (biochemical)

Hili ndilo linalooumiza Zaidi. Kuwa haya yote yanafanywa na binadamu dhidi ya binadamu mwenzie. Sasa mimi na wewe tuendelee kukaa hapa na kuwaza style mbalimbali za kuwaridhisha wanawake na wanaume katika ngono. Tuendelee tu kushabikia vigodoro, tukutane kule forums ya mambo yetu pendwa. mambo rahisi na laini laini tu. tuwekeze katika style hizi za katerero, punda afe,mbuzi kagoma, kitambaa cheupe n.k tuendelee kufuatilia msanii gani anatembea na nani.

Tuendelee kusumbuana kwa mambo ya kipuuzi. Siku ikifika hatujui hata jinsi ya kutengeneza mask… tutakufa kama kumbikumbi. Hapo ndipo ninapojisia uvivu wa kuwaza. Naukunyata moto tu na kuugua moyoni. Unajua nini? Najivunia kuwa mwafrika ila nasikitika sana kuzaliwa afrika.
 
Unajua nini? Najivunia kuwa mwafrika ila nasikitika sana kuzaliwa afrika.
Mkuu hata mimi nakuunga mkono hapa najuta kuzaliwa Afrika ya Tanzania. Kwakweli sitaki wanangu waje waishi kwa hili bara aisee wakajuta kama mimi. Ila tuvumilie tu ndo tushakua wa Afrika
 
Kama nisingeona neno mgegedo ningejua watu wamedukia account yako mkuu,

Hiki kitu cha sisi weusi kuwa wasindikizaji kinasikitisha sana

Yaani kila kukicha wenzetu wana mambo mapya sisi bado tunahangaika na makontena ya fulani bandarini.
 
Daah isee na bado tunakauli yetu pendwa "yajayo yana furahisha" sasa kama mambo yenyewe ndio hayo mbona kazi ipo
 
Ha ha! mkuu ulitaka binadamu ajishugulishe kupambana na kifo..?
nafasi ya kututosha haipo!.. umeandika hayo yote,unafikiri mwanadamu anastahiri kuwepo au asiwepo..?
kuuwana si jambo zuri ndio lkn kilichojaa ndani yetu tunakionyesha nje yetu!,tutaungana siku tukipata adui mmoja lkn hayupo adui anaetufanya tuungane tumpige,huyo wanaemuita shetani ni adui asieonekana wakuimagne! ndio maana tunabutuana sisi kwa sisi!.
watengeneze siraha tu what we show is the reality of human being.. tunatembea ktk misingi ya kimazingira,tumeratibiwa ni juhudi yako sasa kuuona usahihi ama usio usahihi
 
Iwe kwa drones au hizo kemikali utakufa, lakini pia hata bila hizo drones na hayo makemikali bado utakufa...

Ufuatilie habari za mastaa, utakufa na usipofuatilia habari za mastaa pia utakufa...

Ugegedane utakufa, na usipogegedana pia utakufa...

Kwahiyo, kufa kupo tu mkuu GuDume
 
technolojia na kifo kipi kimeanza..? ukishatafakari hapo basi utaona ni jinsi gani mwenyezi mungu alivyo mbele zaidi kwa mahatua tillions ya ufikiri baina ya mwanadamu na yeye..... kivyovyote vile only death ndio haki iliyo sawa kwa wanadamu wote bila kujali madaraja ya ubora wao hapa ulimwenguni...
uvumbuzi wa hizo technology ni utashi wa mwanadamu ktk matumizi ya akili aliyojaaliwa na mwenyezi mungu.....kutojishughurisha na uvumbuzi wa vifaa angamizi dhidi yetu binadamu haimanishi kuleta uwezekano wa kukiepuka kifo.......
 
ndugu tulia tu soma kwa umakini aya baada ya aya utagundua nlichokuwa nazungumzia. leo nmetumia lugha nyepesi sana.. mana haya yooooote nilikuwa najadiliana na mtoto wangu kumuelezea kuwa anapaswa afanye kitu flani. asiwe msindikizaj. ni mbaya sana kifo kukukuta umekaa unakisubiri.. hapo unakuwa umeshakufa mara nyingi na kwa kishindo kikuu. watu jasiri bado hupambana na kifo na wakati mwingine hushinda.

technolojia na kifo kipi kimeanza..? ukishatafakari hapo basi utaona ni jinsi gani mwenyezi mungu alivyo mbele zaidi kwa mahatua tillions ya ufikiri baina ya mwanadamu na yeye..... kivyovyote vile only death ndio haki iliyo sawa kwa wanadamu wote bila kujali madaraja ya ubora wao hapa ulimwenguni...
uvumbuzi wa hizo technology ni utashi wa mwanadamu ktk matumizi ya akili aliyojaaliwa na mwenyezi mungu.....kutojishughurisha na uvumbuzi wa vifaa angamizi dhidi yetu binadamu haimanishi kuleta uwezekano wa kukiepuka kifo.......
 
ndugu tulia tu soma kwa umakini aya baada ya aya utagundua nlichokuwa nazungumzia. leo nmetumia lugha nyepesi sana.. mana haya yooooote nilikuwa najadiliana na mtoto wangu kumuelezea kuwa anapaswa afanye kitu flani. asiwe msindikizaj. ni mbaya sana kifo kukukuta umekaa unakisubiri.. hapo unakuwa umeshakufa mara nyingi na kwa kishindo kikuu. watu jasiri bado hupambana na kifo na wakati mwingine hushinda.

Ha ha! mkuu ulitaka binadamu ajishugulishe kupambana na kifo..?
nafasi ya kututosha haipo!.. umeandika hayo yote,unafikiri mwanadamu anastahiri kuwepo au asiwepo..?
kuuwana si jambo zuri ndio lkn kilichojaa ndani yetu tunakionyesha nje yetu!,tutaungana siku tukipata adui mmoja lkn hayupo adui anaetufanya tuungane tumpige,huyo wanaemuita shetani ni adui asieonekana wakuimagne! ndio maana tunabutuana sisi kwa sisi!.
watengeneze siraha tu what we show is the reality of human being.. tunatembea ktk misingi ya kimazingira,tumeratibiwa ni juhudi yako sasa kuuona usahihi ama usio usahihi
 
ndugu tulia tu soma kwa umakini aya baada ya aya utagundua nlichokuwa nazungumzia. leo nmetumia lugha nyepesi sana.. mana haya yooooote nilikuwa najadiliana na mtoto wangu kumuelezea kuwa anapaswa afanye kitu flani. asiwe msindikizaj. ni mbaya sana kifo kukukuta umekaa unakisubiri.. hapo unakuwa umeshakufa mara nyingi na kwa kishindo kikuu. watu jasiri bado hupambana na kifo na wakati mwingine hushinda.

tupambane na maisha kidunia kama tutaishi milele na tupamabane na maisha kiimani kama tutakufa kesho....
 
ndugu tulia tu soma kwa umakini aya baada ya aya utagundua nlichokuwa nazungumzia. leo nmetumia lugha nyepesi sana.. mana haya yooooote nilikuwa najadiliana na mtoto wangu kumuelezea kuwa anapaswa afanye kitu flani. asiwe msindikizaj. ni mbaya sana kifo kukukuta umekaa unakisubiri.. hapo unakuwa umeshakufa mara nyingi na kwa kishindo kikuu. watu jasiri bado hupambana na kifo na wakati mwingine hushinda.
Usidhani sijakuelewa lkn nimesimamia ktk mantiki ya mazingira na ndio maana nikauliza,kutokana na binadamu kujiangamiza na kuangamiza mazingira unafikiri anastahiri kuwepo au lah..?
 
good question.. binadamu anastahili kuwepo ila anastahili kutengeneza mazingira mazuri zaidi ya kumfanya yeye kuwepo hapa duniani.. binadamu angewekeza zaidi katika kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi hapa duniani kuliko ya kuondoleana uhai na kuharibu mazingira ... nadhani turudi kuishi Eden.

Usidhani sijakuelewa lkn nimesimamia ktk mantiki ya mazingira na ndio maana nikauliza,kutokana na binadamu kujiangamiza na kuangamiza mazingira unafikiri anastahiri kuwepo au lah..?
 
Tuendelee kusumbuana kwa mambo ya kipuuzi. Siku ikifika hatujui hata jinsi ya kutengeneza mask… tutakufa kama kumbikumbi. Hapo ndipo ninapojisia uvivu wa kuwaza. Naukunyata moto tu na kuugua moyoni. Unajua nini? Najivunia kuwa mwafrika ila nasikitika sana kuzaliwa afrika.

Mara nyingi hizo huwa ni mbwembwe tu lkn uhalisia wa Vita ni mwingine kabisa, hakuna nchi Dunia hii iliyokuwa na advanced technology kama Nazi Germany, lkn walishindwa Vita, hivyo kwenye Vita kuna mambo mengi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom